Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Prussia Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Prussia Mashariki (nyekundu) katika mipaka ya Ujerumani ya 1871-1919.
Prussia mashariki na mipaka ya Ujerumani 1919-1945
Prussia Mashariki katika mipaka ya 1923 hadi 1939

Prussia Mashariki (jer. Ostpreußen, ing. East Prussia, pol. Prusy Wschodnie) ilikuwa jimbo la kihistoria katika dola la Prussia katika Ujerumani hadi mwaka 1945. Leo hii eneo lake limegawiwa kati ya mkoa wa Kaliningrad wa Urusi na mkoa wa Warmia i Mazury katika Poland.

Prussia Mashariki ilikuwa chanzo cha Prussia yenyewe; tangu kuunganishwa na utemi wa Brandenburg ilikuwa tu jimbo la Mashariki. Mji mkuu ukawa Königsberg iliyoitwa leo hii kwa jina la Kirusi Kaliningrad.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na kuanishwa upya kwa dola la Poland Prussia Mashariki ilikuwa eneo la Kijerumani lisilo na njia ya moja kwa moja na nchi mama lakini mawasiliano wote yalikuwa kwa njia ya reli kupitia Poland au kwa njia ya bahari Baltiki.

Washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia walimaua kutenganisha jimbo hili na Ujerumani na kuigawa kati ya Poland na Urusi. Wenyeji wazalendo karibu wote walikimbia au walifukuzwa baada ya vita, kwa jumla watu milioni 2.5; wengi walikufa walipokimbia katika majira baridi ya Januari na Februari 1945.

Mwaka 1990 Ujerumani uliounganishwa tena ulikubali mipaka iliyotokea baada ya vita katika mapatano ya kimaaifa.

Tangu 1946 kaskazini ya Prussia Mashariki inaitwa Kaliningrad Oblast ikiwa mkoa wa Urusi. Kusini ya Prussia Mashariki ni mkoa wa Poland kwa jina la Warmia-Masuria.