Salomon Kalou
Youth career | |||
---|---|---|---|
–2000 | Mimosas | ||
Senior career* | |||
Miaka | Timu | Apps (Gls)† | |
2000–2003 | Mimosas | 14 (12) | |
2003–2006 | Feyenoord | 65 (35) | |
2004 | → Excelsior (loan) | 10 (4) | |
2006– | Chelsea | 100 (20) | |
Timu ya Taifa ya Kandanda‡ | |||
2007– | Côte d'Ivoire | 17 (9) | |
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 12:42, 21 Novemba 2009 (UTC). † Appearances (Goals). |
Salomon Kalou (alizaliwa Oumé, Côte d'Ivoire, 5 Agosti 1985) ni mchezaji wa kandanda kutoka Ivory Coast, ambaye sasa anasakata kabumbu katika kilabu ya Chelsea na zamani alikuwa anachezea kilabu ya Kiholanzi ya Feyenoord.
Yeye ni mshambulizi, lakini mara nyingi hutumika kama winga akiichezea Chelsea. Anapendelea kucheza upande wa kushoto kwa uwanja kwani upande huu humpa fursa kuingia ndani ya boksi na kuchapa kombora kutumia mguu wake wa kulia.
Wasifu wa Klabu
[hariri | hariri chanzo]Ivory Coast na Uholanzi
[hariri | hariri chanzo]Kama kaka yake, Kalou alianza wasifu wake wa klabu katika klabu ya mtaa ya Mimosas kabla ya kwenda kucheza kandanda katika nchi za Ulaya. Mkufunzi wa Auxerre, Guy Roux, alitaka kumsaini ili aungane na kakake, mchezaji wa kitambo wa Feyenoord, Bonaventure Kalou. Kalou alitia saini mkataba wa klabu ya Excelsior Rotterdam, klabu ndogo ya Feyenoord Rotterdam.
Kalou alifunga mabao 15 katika matokeo 11 akiichezea Excelsior miaka ya 2002 hadi 2003. Alipandishwa cheo hadi Feyenoord na alicheza katika kiwango cha juu cha ligi ya Kiholanzi kwa misimu mitatu kuanzia mwaka wa 2003 hadi mwaka wa 2006. Katika wakati wake akiwa Feyenoord, Salomon alifunga mabao 35 katika matokeo 67 ya ligi katika klabu hiyo ya Rotterdam, na pia alishinda tuzo ya kibinafsi aliposhinda tuzo la Johan Cruijff mwaka wa 2005 kwa kuwa kijana mwenye talanta ya kuahidi msimu huo.
Kushindwa kupata uraia wa Kiholanzi
[hariri | hariri chanzo]Kalou alipokea makini kutoka kwa vyombo vya habari kuhusu uwezekano wake kuwa raia wa Uholanzi , ambao kama uraia huo ungekubaliwa, ungempa fursa ya kuchezea timu ya taifa ya kandanda ya Uholanzi. Kalou hakuwahi kuichezea timu ya kandanda ya Côte d'Ivoire, na hii ingempa ukastahiki kuichezea timu ya taifa ya kandanda ya Uholanzi kama angepata uraia huo. Kakake Bonaventure alimwagiza atafute uraia wa kigeni baada ya kupata matatizo ya mara kwa mara na wasimamizi wa kandanda ya Cote d'Ivoire.
Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Marco van Basten, anamchukulia Kalou kama mchezaji mwenye talanta kubwa, hivyo basi maombi rasmi yalifanywa kwa haraka. Hata hivyo Waziri wa Uhamiaji, Rita Verdonk alikataa kuzingatia kuharakishwa kwa mchakato ambao ungemfanya Kalou awe raia wa Uholanzi.
Van Basten, ambaye alikuwa na nia ya kuonyesha thamani ya Kalou katika timu ya taifa ya Kiholanzi, aliungwa mkono na washawishi wakubwa wa kandanda, akiwemo legend wa kandanda ya Uholanzi,Johan Cruyff. Ingawa makubaliano ya jumla kati ya wenye busara wa kandanda kwamba Kalou atakuwa na thamana kubwa kwa timu ya Uholanzi, Verdonk alikataa ombi la kufikiria upya suala hilo. Baadaye Cruyff alitoa maoni kuwa huenda timu ya taifa ya Kiholanzi ingefanikiwa zaidi iwapo Kalou angepata uraia wa Kiholanzi.
Kalou alitoa wito kutokana na uamuzi huo na akapeleka suala hilo katika mahakama ya sheria, ambapo alipata ushindi tarehe 9 Desemba 2005 wakati jaji alimwamuru Verdonk kufikiria upya kama Kalou angeweza au asingeweza kupata uraia kwa haraka. Verdonk aliamua kukata rufaa, kwa kupeleka suala hilo mbele ya Baraza la Serikali. Kalou alisema hadharani kuwa alikuwa amepoteza matumaini ya kupata uraia wa Kiholanzi.
Kitambulisho cha Centraal Beheer
[hariri | hariri chanzo]Mchakato wa Kalou kupata uraia wa Kiholanzi ulikuwa mandhari ya kitambulisho fupi ya runinga kwa Centraal Beheer. Katika kitambulisho hicho cha Aprili 2006, mtu aliyekuwa anaashiria Kalou anaonyeshwa akipata uraia, lakini si ya Uholanzi bali ya Ujerumani.
Kitambulisho hiki pia kilikuwa kinaashiria mshambulizi aliyezaliwa Angola, Nando Rafael, ambaye sasa anaichezea timu ya Aarhus GF, ambaye pia alishindwa kupata uraia wa Kiholanzi alipokuwa anaichezea klabu ya Ajax,.Alihamia klabu ya Hertha Berlin ya ligi ya Bundesliga huko Ujerumani, akawa raia wa Kijerumani, na akaiwakilishwa Ujerumani katika mashindano ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21.
Kalou hakufurahishwa na kitambulisho hiki, na sheria ya hakimiliki ikiwa mikononi mwake, kitambulisho hicho kiliondolewa katika runinga ya Kiholanzi wiki hiyo hiyo.
Chelsea
[hariri | hariri chanzo]Msimu wa 2006/07
[hariri | hariri chanzo]Kalou alihamia Chelsea mnamo 30 Mei 2006, kwa ada ambyo haikutajwa, lakini iliaminika kuwa zaidi ya paundi (£) milioni 9. Chini ya mkataba na Chelsea hadi mwaka wa 2009, Kalou alipewa jesi lenye namba 21.
Meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho alimsifu mchezaji huyu kutoka Ivory Coast kama kijana mwenye bidii,anayeweza kufanya vitu vingi, mwenye nia ya kuboreka, na asiye na uwoga.. Kalou alikiri kwamba alileta kamera katika mazoezi yake ya kwanza katika kituo cha mafunzo cha Chelsea kilicho Cobham kwa sababu hakuweza kuamini kwamba atakuwa anacheza na wachezaji maarufu kama Michael Ballack, John Terry na Didier Drogba. Akielezea uzoefu huo , Kalou alisema:
"Hii ilikuwa ndoto ya maisha yangu na sikutaka kuamka na kutambua kuwa haikuwa kweli."
Kulingana na Soccernet, Kalou alibaini kuwa mchezaji ambaye alikuwa anataka kumuiga alikuwa mshambulizi wa Ufaransa na mshikilia rekodi ya mabao katika klabu ya Arsenal ,Thierry Henry, wa Barcelona, na hujaribu kuiga ujuzi wa Henry akipata nafasi. Mapenzi yake kwa mchezo wa Henry ulikuwa sababu ya uamuzi wake wa kucheza katika ligi kuu ya Uingereza, kwani ni ligi hii ambayo Henry alikuwa nyota.
Akiwa Chelsea, Kalou hucheza na mwenzake, nahodha wa Côte d'Ivoire Didier Drogba. Kalou alifunga mabao yake ya kwanza ya Chelsea katika mechi dhidi ya Portsmouth kwa kufunga mabao tatu na kupewa mpira uliyotumiwa katika mechi hiyo ambayo walishinda 5-0. Kalou alifunga bao lake la kwanza la timu kuu ya Chelsea katika mechi ambayo walishinda kwa mabao mawili dhidi ya Blackburn Rovers katika raundi ya tatu ya Kombe la Carling.
Kalou alifunga bao lake la kwanza la ligi kuu ya Uingereza mwezi wa Desemba mwaka wa 2006, mechi ambayo Chelsea ilishinda 3-2 dhidi Wigan Athletic katiak uwanja wa JJB. Alifunga bao lake la pili la ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Blackburn, mechi ambayo Chelsea ilishinda 3-0. Pia alifunga bao katika dakika ya 93 dhidi ya Watford na kuiweka Chelsea 1-0 juu. Pia alifunga bao maridadi kutoka yadi 12 dhidi ya Tottenham Hotspur katika robo fainali ya Kombe la FA, iliyomalizika 3-3. Chelsea ilishinda mechi ya marudiano 1-2 ,kabla ya kuishinda Blackburn Rovers 2-1 na kupata fursa ya kucheza katika fainali. Kalou pia aliingia kama mbadala katika fainali ya kombe la FA mwaka wa 2007, mechi ambayo waliishinda Manchester United na kumpa kombe lake la pili nchini Uingereza, Awali aliingia kama mbadala katika fainali ya Kombe la Carling mwaka wa 2007 dhidi ya Arsenal, mechi ambayo Chelsea ilishinda 2-1.
Msimu wa 2007/08
[hariri | hariri chanzo]Kalou aliendeleza fomu yake nzuri msimu uliyofuata, kwa kufunga bao lake la kwanza la kampeni mpya dhidi ya Manchester City, mechi ambayo Chelsea ilishinda 6-0 katika uwanja wa Stamford Bridge na pia kufunga bao la ufunguzi dhidi ya Derby County,mechi ambayo Chelsea ilishinda 2-0. Salomon Kalou aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aiyeotea sana kwa idadi ya maoteo 107 katika mechi 30; hivyo basi kuisaliti uwezo wake wa kuweza kuisoma mchezo.
Robo fainali ya Kombe la Carling ya mwaka wa 2007-2008 Kalou alicheza upande wa kulia ya mfumo wa 4-3-2-1. Kalou alijitengenezea na kuwatengenezea wachezaji wenzake wa Chelsea nafasi nyingi; hii ilikuwa pamoja na krosi muruwa, iliyochanglia Shevchenko kufunga bao la kichwa. Baadaye alifunga mabao dhidi ya Newcastle United na Fulham na kuchangia mafanikio Chelsea. Alifunga mabao dhidi ya West Ham United, Olympiacos na Derby County. Krosi yake ndani ya boksi dakika ya mwisho ilisababisha John Arne Riise kujifunga bao katika nusu fainali ya kwanza ya kombe la mabingwa barani Ulaya la UEFA katika uwanja wa Anfield. . Kalou pia alifunga penalti ya sita katika fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya Manchester United mjini Moscow, mechi ambayo Chelsea ilipoteza.
Msimu wa 2008/09
[hariri | hariri chanzo]Hakucheza chini ya halifa wa Avram Grant, Luiz Felipe Scolari isipokuwa katika mechi za mazoezi kabla ya msimu kuanza. Hii ilikuwa kwa sababu ya ushiriki wake katika michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka wa 2008 kwani alikuwa katika kikosi cha kandanda cha Ivory Coast ambacho kilikuwa na vijana wasiokuwa na umri zaidi ya 23. Hata hivyo aliingia kama mbadala dhidi ya Manchester United tarehe 21 Septemba 2008 na alifunga bao la kichwa dakika ya 80 kutoka krosi ya John Obi Mikel. Bao hilo lilihakikisha kuwa Chelsea lilipata angalau pointi moja na kuadhimisha rekodi yao ya kutoshindwa nyumbani. Kalou kisha alifunga mabao mawili na kumwandalia pasi Frank Lampard aliyefunga kwa kichwa tarehe 18 Oktoba 2008,mechi ambayo Chelsea ilishinda 5-0 dhidi ya Middlesbrough ugenini. Alifunga tena mabao mawili dhidi ya Middlesbrough, lakini wakati huu alikuwa nyumbani katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 28 Januari 2008, mechi ambayo Chelsea ilishinda 2-0.Chini ya meneja Guus Hiddink alicheza mechi zaidi. Mnamo 25 Aprili 2009, alifunga bao la ushindi dhidi ya West Ham United.
Msimu wa 2009/10
[hariri | hariri chanzo]Kalou na Chelsea walianza msimu kwa ushindi; waliishinda Manchester United na kuinua kombe la Community Shield la FA mwaka wa 2009 huku Kalou akifunga bao la ushindi na kusherekea siku yake ya kuzaliwa wiki hiyo hiyo. Kalou alifunga bao lake la kwanza la msimu wa 2009/10 dhidi ya Queens Park Rangers katika uwanja wa Stamford Bridge katika raundi ya 3 ya kombe la Carling, na kuipatia timu yake ushindi uliyostahili wa 1-0. Tarehe 12 Oktoba 2009, Kalou alisaini mkataba mpya wa miaka 3 wa Chelsea, ambayo inamfunga kuwa mchezaji wa Chelsea hadi mwaka wa 2012.. Alisherehekea mkataba wake mpya kwa kufunga mabao mawili dhidi Club Atletico de Madrid katika kombe la mabingwa barani Ulaya la UEFA na hivyo basi kuisaidia Chelsea kudumisha rekodi yake ya asilimia 100 katika shindano hilo. Kalou aliendeleza fomu yake nzuri kwa kufunga bao kwa kichwa katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Bolton katika kombe la Carling.
Maisha ya binafsi
[hariri | hariri chanzo]Kalou ana kaka watano na dada wanane na hawa wote ni wa mama mmoja Kakake, Bonaventure Kalou, pia anacheza kandanda ya utaaluma, na kwa sasa anaichezea timu ya Heerenveen kutoka Uholanzi.
Wasifu wa Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Katika kombe la dunia la FIFA la mwaka wa 2006, Uholanzi na Ivory Coast waliwekwa katika kundi moja katika raundi ya kwanza. Kama Kalou angepata uraia wa Kiholanzi na kuchaguliwa kuiwakilisha timu ya Uholanzi, angecheza dhidi ya nchi yake ya kuzaliwa na huenda pia angecheza dhidi ya ndugu yake. Kushindwa kwa Kalou kupata uraia wa Kiholanzi kulikuwa sababu ya uamuzi wake kuiacha Feyenoord kwenda Chelsea.
Ametajwa katika kikosi cha taifa cha Cote d'Ivoire mara kadhaa, Hata hivyo yeye alikataa kuiwakilisha timu hiyo hadi tarehe 6 Februari 2007 wakati alicheza mechi yake ya kwanza ambayo ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Guinea, ambayo ”The Elephants”,kama timu hiyo ya Ivory Coast inavyojulikana, ilishinda 1-0. Pia aliiwakilisha timu ya Ivory Coast katika kombe la mataifa barani Afrika na alifunga bao muruwa dhidi ya Nigeria, ambao walitarajiwa kuishinda kombe hilo, katika mechi ya ufunguzi.
Baada ya kushindwa kupata pasipoti ya Kiholanzi, Kalou aliamua kuicheza timu ya Cote d'Ivoire. Bao lake la kwanza la kimataifa lilifungwa tarehe 21 Machi 2007 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mauritius. Alishiriki katka kombe la mataifa barani Afrika mwaka wa 2008, alifunga mabao tatu, na timu yake ilipata nafasi ya 4 baada ya kupoteza mechi dhidi ya Ghana.
Kalou amefunga ndoa na mwanamke Msomali.
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Msimu | Timu | Taifa | Shindano | Ligi | Mabao | Kombe | Mabao | Ulaya | Mabao | Jumla | Mabao |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
2003–04 | Excelsior Rotterdam | Uholanzi | Eerste Divisie | 11 | 4 | - | - | - | - | 11 | 4 |
2003–04 | Feyenoord | Uholanzi | Eredivisie | 2 | 0 | - | - | - | - | 2 | 0 |
2004–05 | Feyenoord | Uholanzi | Eredivisie | 31 | 20 | - | - | 7 | 4 | 38 | 24 |
2005–06 | Feyenoord | Netherlands | Eredivisie | 34 | 15 | - | - | 2 | 0 | 36 | 15 |
2006–07 | Chelsea | Uingereza | Ligi kuu ya Uingereza | 33 | 7 | 13 | 2 | 8 | 0 | 54 | 9 |
2007–08 | Chelsea | Uingereza | Ligi kuu ya Uingereza | 30 | 7 | 3 | 1 | 11 | 1 | 44 | 9 |
2008–09 | Chelsea | Uingereza | Ligi kuu ya Uingereza | 24 | 6 | 7 | 3 | 8 | 1 | 39 | 10 |
2009–10 | Chelsea | Uingereza | Ligi kuu ya Uingereza | 7 | 0 | 3 | 3 | 4 | 2 | 14 | 5 |
Jumla | 172 | 58 | 26 | 9 | 40 | 8 | 238 | 76 |
Mabao ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Salomon Kalou: Mabao ya Kimataifa | ||||||||
# | Tarehe | Ukumbi | Mpinzani | Mabao | Matokeo | Mashindano | ||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | 21 Machi 2007 | Belle vue, Mauritius | Mauritius | 3-0 | Walishinda | Kirafiki | ||
2 | 3 Juni 2007 | Bouaké, Cote d'Ivoire | Madagascar | 5-0 | Walishinda | 2008 Afrika ya Kombe la Mataifa ya kufuzu | ||
3 | 21 Novemba 2007 | Doha Qatar | Qatar | 6-1 | Walishinda | Kirafiki | ||
4 | 12 Januari 2008 | Mji wa Kuwait, Kuwait | Kuwait | 2-0 | Walishinda | Kirafiki | ||
5 | 21 Januari 2008 | Sekondi, Ghana | Nigeria | 1-0 | Walishinda | Kombe la Mataifa ya Afrika 2008 | ||
6 | 3 Februari 2008 | Sekondi, Ghana | Guinea | 5-0 | Walishinda | Kombe la Mataifa ya Afrika 2008 | ||
7 | 3 Februari 2008 | Sekondi, Ghana | Guinea | 5-0 | Walishinda | Kombe la Mataifa ya Afrika 2008 | ||
8 | 11 Oktoba 2008 | Abidjan, Ivory Coast | Madagascar | 3-0 | Walishinda | Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010 |
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Chelsea
- FA Community Shield: 2009
- Kombe la FA: 2007, 2009
- Kombe la Carling: 2007
Kibinafsi
[hariri | hariri chanzo]- Talanta wa Kiholanzi wa mwaka (2005)
- Mchezaji mchanga bora wa mwaka wa CAF - Ivory Coast / Chelsea (2008)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Salomon Kalou career stats kwenye Soccerbase
- Kalou commercial of Centraal Beheer Archived 12 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Ivory Coast in new bid to lure Kalou