Souk Ahras
Souk Ahras (Kiarabu: سوق أهراس; jina la kale Thagaste) ni mji wa Algeria ya kaskazini-mashariki karibu na mpaka wa Tunisia. Idadi ya wakazi ni takriban 150,000. Jina la mji ni mmchanganyiko wa Kiarabu na Kiberberi likimaanisha "soko la simba".
Mji unajulikana kwa jina la kihistoria Thagaste hasa kama mahali alikozaliwa Agostino wa Hippo mnamo mwaka 354 kama mtoto wa Patricius na Monika. Wakati ule ilikuwa mji muhimu wa jimbo la Numidia ndani ya Dola la Roma uliotajwa mara ya kwanza na mwandishi Mroma Plinius Mzee (23-79). Hakuna habari zaidi juuy a mwanzo wa mji.
Wakati wa Agostino ilikuwa mji mwenye askofu na maaskofu walitajwa mjini hadi mwaka 600. Agostino alitaja pia monasteri ndani ya mji.
Katika karne ya 19 mji ulikuwa na walowezi Wafaransa waliokuta wenyeji Waberberi walioogea tayari Kiarabu.
Mji ulikua katika karne ya 20 baada ya njia ya reli kufika na kutokana na migodi iliyochimbwa hapa.