Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Stanislaus mfiadini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Stanislaus.

Stanislaus mfiadini (kwa Kipolandi:Stanisław Szczepanowski; 26 Julai 103011 Aprili 1079) alikuwa askofu wa Kraków[1] kuanzia mwaka 1072 hadi kifodini chake [2].

Kati ya maonevu ya wakati wake, alitetea kwa nguvu zake zote ustaarabu na tunu za Kikristo na kuongoza jimbo lake kama mchungaji mwema akisaidia maskini na kutembelea kila mwaka waklero wake.

Anajulikana hasa kwa kuuawa wakati wa kuadhimisha ibada na mfalme wa Polandi Bolesław II ambaye hakupenda makemeo yake makali.

Kwa sababu hiyo Stanislaus alitangazwa mtakatifu mfiadini na Papa Inosenti IV tarehe 17 Septemba 1253.

Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki kote duniani tarehe ya kifodini chake[3], lakini pia tarehe 7 Mei na 8 Mei, hasa nchini mwake.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Foley O.F.M., Leonard. Saint of the Day, Lives, Lessons, and Feast, (revised by Pat McCloskey O.F.M.), Franciscan Media". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-16. Iliwekwa mnamo 2018-06-24.
  2. Fr. Paolo O. Pirlo, SHMI (1997). "St. Stanislaus". My First Book of Saints. Sons of Holy Mary Immaculate - Quality Catholic Publications. ku. 80–81. ISBN 971-91595-4-5.
  3. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.