Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Ghafi ya tani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tani GT)
Vipimo vya ghafi ya tani hufanywa kwa kupima Ujazo wa Meli kutoka kwenye mkuku wa merikebu mpaka kwenye faneli.

Ghafi ya tani (kifupi: GT; Kiingereza: gross tonnage) ni kipimo cha ukubwa wa meli kilichokuwa kawaida kimataifa tangu mwaka 1982 kufuatana na mapatano ya kimataifa kuhusu upimaji wa ukubwa wa meli (The International Convention on Tonnage Measurement of Ships) ya mwaka 1969. Ghafi ya tani ilichukua nafasi ya vipimo vya awali vilivyoitwa pia tani lakini kwa mjao tofauti iliyokadiria mjao wa nafasi za shehena (mzigo) pekee.

Umuhimu wa ghafi ya tani ni ya kwamba kodi na malipo kwa ajili ya meli hufuata kipimo hiki kama vile kodi za kutumia mifereji (Suez, Panama) au kukaa bandarini.

Ghafi ya tani inataja mjao wa nafasi yote ya ndani ya meli, yaani ya kila sehemu ambayo imefungwa kwa kuta za pembeni, sitaha na majengo juu ya sitaha.

Lakini si mjao huu pekee yake. Idadi ya mita za mjao inazidishwa kwa namba inayotegemea ukubwa wa meli iko kati ya 0.22 na 0.32; yaani hali halisi asilimia 22 hadi 32 ya mjao inahesabiwa kuwa ghafi ya tani. Meli ndogo zinapata makadirio nafuu yaani ya asilimia 22 au karibu nayo halafu meli kubwakubwa hukadiriwa kwa namba inayolingana zaidi na 32.

Meli yenye mjao wa mita za ujazo 10,000 inazidishwa na namba 0.28 hivyo kukadiriwa kuwa na ghafi ya tani 2,800.