Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Teko Modise

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Teko Modise

Teko Modise (alizaliwa katika sehemu ya Soweto, Mkoa wa Gauteng, 22 Desemba 1982) ni mwanakandanda kutoka Afrika Kusini, ambaye anaichezea klabu ya Orlando Pirates inayoshiriki katika Premier Soccer League na timu ya taifa ya Afrika ya Kusini.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Teko Modise Tsholofelo alizaliwa katika sehemu ya Meadowlands, Soweto na alilelewa na mama yake. Yeye ni mzaliwa wa tatu katika familia ya watoto watatu (kaka na dada).

Alipokuwa analelewa kama mtoto alikuwa anaishabikia timu ya Kaizer Chiefs, ambao ni wapinzani wa jadi wa Orlando Pirates.

Wasifu wake wa Uchezaji

[hariri | hariri chanzo]

Alitumia zaidi ya wasifu wake wa katika sehemu ya Limpopo akizichezea klabu za Ria Stars na City Pillars, mtawalia, ambazo sasa hazipo tena.

Alliteuliwa kama Mchezaji wa Msimu wa Mvela Golden League wakati wa alipokuwa akiichezea timu ya City Pillars wakati wa msimu wa 2005/2006.

Katika miaka ya 2008 na 2009, akawa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo la Mwanakandanda wa Mwaka wa PSL .

majuzi Modise aliteuliwa kama balozi maalumu na kampuni ya kimataifa ya McDonald's kwa ajili ya kombw la dunia la FIFA la mwaka wa 2010 na pia kama balozi wa Coca-Cola, Nike, Telkom na Samsung.Teko pia amelengwa na klabu za Ligi ya Uingereza kama vile Aston Villa na Wigan Athletic. Klabu za AC Milan na Inter Milan zinaweza kuwa na nia na shauku ya kugombea Modise katika dirisha ya uhamisho ya majira ya joto baada ya kukamilika kwa msimu wa 2008/2009.

Uvumi zaidi uliendelea wakati wa majira ya joto ya mwaka wa 2009, wakati uvumi ulijitokeza kwamba idadi ya vilabu vilikuwa vinazingatia kumsajili Teko zikiwa ni pamoja na Manchester City, AC Milan, Inter Milan na Birmingham City. Modise aliiambia Sky Sports News kwamba kwamba ingekuwa vigumu kukataa mkataba kutoka timu ya Italia, akiongelea ushawishi wa mwenzake wa kimataifa Steven Pienaar kama sababu muhimu. Hata hivyo, bei ya kuuliza ya paundi (£) milioni 4 ilikuwa kitita kubwa sana.

Wasifu wa Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Modise aliichezea timu ya Afrika Kusini kwa mara ya kwanza wakati wa kombe la COSAFAmwaka wa 2007. Alicheza mechi yake ya kwanza na timu mwandamizi mnamo 26 Mei 2007 dhidi ya Malawi. Alijumuishwa katika orodha ya Afrika Kusini ya wachezaji watakao shiriki katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ghana. Pia hujulikana kama Jonas Andersen. Kwa sasa ameichezea timu mwandamizi ya Afrika Kusini mechi 33 na amefanikiwa kufunga mabao 9. Modise amekuwa mchezaji muhimu katika mechi nyingi za kimataifa za Bafana Bafana. . Mwaka wa 2008 aliteuliwa kama mchezaji bora wa barani Afrika wakati wa msimu.

Modise alikuwa katika kikosi cha Afrika Kusini kilichoshinda kombe la COSAFA mwaka wa 2007.

Hakupata nafasi kuziwakilisha timu zozote za kitaifa za Afrika Kusini za kikomo cha umri. Mnamo 14 Juni 2009, alituzwa tuzo la Budweiser la mchezaji bora wa mechi katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Shirikisho la FIFA mwaka wa 2009 dhidi ya Iraq.

Mabao ya kimataifa

[hariri | hariri chanzo]
# Tarehe Ukumbi Mpinzani Pointi Tokeo Mashindano
[1] 2007/05/27 Lobamba, Swaziland Mauritius 1-0 2-0 Kombe la COSAFA
2 2007/05/27 Lobamba, Swaziland Mauritius 2-0 2-0 Kombe la COSAFA
3 2007/09/29 Atteridgeville, Afrika Kusini Botswana 1-0 1-0 Kombe la COSAFA
4 2007/11/20 Durban, Afrika Kusini Kanada 1-0 2-0 Mechi ya kirafiki
5 2007/11/20 Durban, Afrika Kusini Kanada 2-0 2-0 Mechi ya kirafiki
6. 2008/08/19 London, Uingereza Australia 2-2 2-2 Mechi ya kirafiki
7 2008/11/19 Rustenburg, Afrika Kusini Kamerun 1-0 3-2 Mchuano wa Nelson Mandela
8 2008/11/19 Rustenburg, Afrika ya Kusini Kamerun 2-0 3-2 Mchuano wa Nelson Mandela
9 2009/01/27 Atteridgeville, Afrika ya Kusini Zambia 1-0 1-0 Mechi ya kirafiki

Kombe la Telkom Charity: 2008

Timu ya Kitaifa

[hariri | hariri chanzo]
  • Kombe la COSAFA: 2007

Tuzo binafsi kuu

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]