Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Mbweta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Telophorus)
Mbweta
Mbweta rangi-tatu
Mbweta rangi-tatu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Malaconotidae (Ndege walio na mnasaba na mbweta)
Jenasi: Chlorophoneus Cabanis, 1850

Malaconotus Swainson, 1824
Telophorus Swainson, 1832

Spishi: Angalia katiba.

Mbweta ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Chlorophoneus, Malaconotus na Telophorus katika familia Malaconotidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Ndege hawa wana rangi kali kwenye kidari na tumbo, k.m. nyekundu, machungwa, njano au kijani. Mgongo wao ni rangi ya majani au zeituni kwa kawaida. Wana domo nene lenye ncha kwa kulabu. Hula wadudu hasa na vertebrata wadogo pia, mijusi kwa kawaida. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini na jike huyataga mayai 2-4.