Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Tendo la ndoa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu mapendo

Moyo katika mapokeo ya Ulaya
ni mchoro unaowakilisha mapendo.
Vipengele Msingi
Mapendo kadiri ya sayansi
Mapendo kadiri ya utamaduni
Upendo (fadhila)
Upendo safi
Kihistoria
Mapendo ya kiuchumba
Mapendo ya kidini
Aina za hisia
Mapendo ya kiashiki
Mapendo ya kitaamuli
Mapendo ya kifamilia
Mapendo ya kimahaba
Tazama pia
Mafungamano ya binadamu
Jinsia
Tendo la ndoa
Maradhi ya zinaa
Siku ya wapendanao

Tendo la ndoa (pia: ngono) ni kitendo cha kujamiiana kati ya mwanamke na mwanamume.

Mkamilishano

[hariri | hariri chanzo]

Jinsia zinalenga kukamilishana katika ndoa. Kadiri ya Biblia Mungu baada ya kumuumba Adamu alisema, “Si vema mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwa 2:18).

Umbile la mwanamume linaelekea kukamilishana na lile la mwanamke kiroho na kimwili. Lakini roho haionekani, hivyo ni rahisi zaidi kuona jinsi miili yao inavyofaa kuungana iwe mwili mmoja.

Hata hivyo tuelewe mkamilishano huo unafanyika katika nafsi pia, ambazo zina vipawa tofauti vinavyowezesha kwa pamoja kukabili vizuri maisha ya nyumbani, ya uchumi, ya siasa, ya dini n.k.

Tukiangalia viungo vya uzazi vya kike tunakuta kwenye kilango chake kizinda, yaani nyama nyembamba inayoondolewa na mwanamume wa kwanza anayekiingilia. Ndiyo sababu ni kama mhuri wa ubikira wa mwanamke. Katikati ya kizinda kuna tundu dogo tu kupitishia damu wakati wa hedhi, yaani siku zile ambazo anatokwa damu kupitia uke ulio nafasi ya wazi (kati ya kizinda na tumbo la uzazi) iliyo tayari kupokea uume na mbegu zake.

Hizo zinasafiri muda wa saa sita hivi katika tumbo la uzazi ili kukifikia kijiyai katika mrija unaoliunganisha na kifuko cha kijiyai. Mbegu zinazofunga safari hiyo zinaweza kuwa milioni kadhaa, lakini chache tu zitafika; tena kati yake, moja tu itapenya kijiyai, kwa sababu mara tu inapoingia kijiyaji kinakuwa kigumu kwa nje, hivi kwamba mbegu nyingine zitagonga bure. Ikiwa mbegu hiyo inabeba kromosomu Y mtoto atakuwa wa kiume, la sivyo atakuwa wa kike.

Mbegu na kijiyai vinapounganika, viini vya urithi vinavyobebwa navyo vinachanganyikana kwa namna mojawapo kati ya zile zote zinazowezekana. Kwa kawaida viini hivyo ni 46 kwa kila binadamu, na kila seli ya mwili wake inavyo. Katika viini hivyo zimo jeni 25,000 hivi, yaani sifa zote za mtu huyo maalumu tangu atungwe hadi afe.

Viini hivyo vinaongoza ujenzi wa mwili kwanza tumboni mwa mama, halafu utengenezaji wa seli mpya baada ya kuzaliwa. Hata mbegu zote zina viini hivyo vya baba, na vijiyai vyote vina viini hivyo vya mama, isipokuwa katika kukomaa vinapungua na kubaki 23 tu kusudi mbegu na kijiyai vikiungana mimba inayopatikana iwe na viini 46 kama kawaida.

Kutokana na wingi usiohesabika wa namna ambazo jeni hizo zinaweza kuchanganyikana, hakuna mtu aliye sawa na mwingine, kama vile alama za vidole zilivyo tofautitofauti. Hivyo toka mwanzo mimba hiyo ni mtu wa pekee, ingawa ina seli moja tu. Seli hiyo itakua na kuanza kugawanyika katika seli 2, 4, 8, 16 n.k.

Ingawa kila moja ina viini vilevile, polepole seli zinatofautiana ili kufanya kazi maalumu (ubongo, moyo na viungo vingine) na kushirikiana zote vizuri katika umoja wa mwili. Baada ya miezi miwili viungo vyote vimeshatengenezwa, halafu vinazidi kukua na kukamilika hadi mwezi wa tisa ambapo mwishoni mwake mtoto atazaliwa.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tendo la ndoa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.