Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Thobias Minzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Thobias Minzi (alizaliwa kijiji cha Iseni katika mkoa wa Mwanza, kaskazini mwa Tanzania, 1984) [1], mbali na kuwa mchoraji maarufu na ni mtengezaji filamu ambaye hutumia namna yake ya kisanii kutoa kazi sanifu. Ni mmoja kati ya wasanii walioweza kujizolea sifa za kuongeza ubunifu katika sanaa za uoni, kitu ambacho kilimpatia tuzo kutoka kwa Rangery Gall.

Minzi alianza shule ya msingi mnamo mwaka 1994 katika shule ya Iseni.

Mwaka 2000 Minzi alifanikiwa kuhitimu elimu ya msingi[2] akasafiri kutokea jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya sanaa ya uchoraji.

Mnamo mwaka 2002, Minzi alijiunga na kundi la wapaka rangi liitwalo Namanga Art Studio. [3]

Minzi aliweza kutengeneza namna ya kisanaa ya kutumia uzi na nguo kufikisha picha na hisia. Michoro ya Minzi inaonyesha wanawake na watoto, majukumu wanayoyafanya katika Maisha ya kila siku ya kiafrika pamoja na changamoto wanazozikumba na kukabiliana nazo katika nchi zinazoendelea. [4]

  1. https://rbb85.wordpress.com/2012/05/15/thobias-minzi/
  2. http://afrum.com/index.php?hash_del=9115472a1427c040579ee95b73873ce4&categ=fam&action=vypis&select=78
  3. http://afrum.com/index.php?hash_del=9115472a1427c040579ee95b73873ce4&categ=fam&action=vypis&select=78
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-08. Iliwekwa mnamo 2019-04-08.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thobias Minzi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.