Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Wakopti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ukristo wa Kikopti)
Msalaba wa Kikopti wenye maandishi asili yanayosema: 'Yesu Kristo, Mwana wa Mungu'.
Picha ya Kikopti ya Mwinjili Marko, anayehesabiwa kuwa mwanzilishi wa Kanisa la Misri.
Rais Nasser wa Misri akipokea ujumbe wa Maaskofu wa Kikopti (1965).
Kanisa la Mt. Marko huko Bellaire, Texas, Marekani. Wakopti milioni 4 wanaishi nje ya Misri.

Wakopti (au Wakhufti) ni Wakristo asili wa Misri, ambao wanafuata madhehebu ya pekee katika kundi la Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki na wanaunda kundi kubwa zaidi la wakazi wasio Waislamu katika nchi hiyo[1][2][3][4][5][6] .

Patriarki wao ni Papa Tawadros II, akiwa na makao makuu jijini Cairo.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Aina hiyo ya Ukristo ilikuwa anaongoza kabisa kati ya dini za Misri kuanzia karne ya 4 hadi karne ya 6 B.K., lakini baada ya uvamizi wa Waarabu (641), Uislamu ulizidi kuenea kwa njia mbalimbali[7].

Hata hivyo, Wakopti wanabaki asilimia 10-20 ya Wamisri wote[8], isipokuwa wanazungumza Kiarabu, si Kikopti tena, ambacho kinatumika tu katika liturujia.

Wakopti wengine wana ushirika kamili na Kanisa Katoliki, na wengine tena ni Waprotestanti.

Jina Kopti linatokana na Kigiriki Αἰγύπτιος, "Egyuptios", yaani "Mmisri".

Kati ya watakatifu muhimu zaidi wa Kikopti kuna mmonaki Antoni Abati na maaskofu Atanasi wa Aleksandria na Sirili wa Aleksandria.

Mchango mkubwa zaidi walioutoa ni kuanzisha umonaki na kutetea umungu wa Yesu Kristo pamoja na usahihi wa kumuita Bikira Maria "Mama wa Mungu".

Kutoka Misri, Ukristo wa aina hiyo ulienea tangu zamani hasa Sudan, Ethiopia na Eritrea.

Siku hizi Wakopti wengi wanazidi kuhamia nchi nyingine, hasa za Magharibi[9].

Jumla yao imekadiriwa kuwa milioni 18-22.[10][11][12]

  1. Youssef, Abdel Rahman. "Egyptian Copts: It’s All in the Number", 30 September 2012. Retrieved on 5 April 2016. Archived from the original on 2016-03-04. 
  2. "Egyptian Copts reject population estimate". Ahram Online. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-29. Iliwekwa mnamo 5 Aprili 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "The Coptic Orthodox Church in action – Al-Ahram Weekly". weekly.ahram.org.eg. Iliwekwa mnamo 2016-05-06.
  4. Cairo, Jared Malsin in (2015-02-20). "'We want our sons back': fears grow for Egyptians missing in Libya". the Guardian. Iliwekwa mnamo 2016-05-06.
  5. "Egypt must help its poor in response to Libya beheadings, economists say". america.aljazeera.com. Iliwekwa mnamo 2016-05-06.
  6. "Egyptian Copts: It’s All in the Number", Al-Akhbar English, 30 September 2012. Retrieved on 8 March 2015. Archived from the original on 2016-03-04. 
  7. Ibrahim, Youssef M.. "U.S. Bill Has Egypt's Copts Squirming", The New York Times, 18 Aprili 1998. Retrieved on 2008-10-08. 
  8. Cole, Ethan (8 Julai 2008). "Egypt's Christian-Muslim Gap Growing Bigger". The Christian Post. Iliwekwa mnamo 2008-10-02.
  9. El-Hennawy, Noha. "EGYPT: Coptic diaspora spreads the word", 24 June 2008. Retrieved on 5 April 2016. 
  10. "Egypt". The World Factbook. American Central Intelligence Agency (CIA). 30 Machi 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-26. Iliwekwa mnamo 5 Aprili 2016. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Abaza, Khairi; Nakhla, Mark (25 Oktoba 2005). "The Copts and Their Political Implications in Egypt". Washington Institute for Near East Policy. Iliwekwa mnamo 5 Aprili 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Morrow, Adam (24 Aprili 2006). "Egypt: Attacks Raise Fear of Religious Discord". Inter Press Service. Iliwekwa mnamo 5 Aprili 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Capuani, Massimo et al. Christian Egypt: Coptic Art and Monuments Through Two Millennia (2002) excerpt and text search
  • Courbage, Youssef and Phillipe Fargues. Judy Mabro (Translator) Christians and Jews Under Islam, 1997.
  • Ibrahim, Vivian. The Copts of Egypt: The Challenges of Modernisation and Identity (I.B. Tauris, distributed by Palgrave Macmillan; 2011) 258 pages; examines historical relations between Coptic Christians and the Egyptian state and describes factionalism and activism in the community.
  • Kamil, Jill. Coptic Egypt: History and a Guide. Revised Ed. American University in Cairo Press, 1990.
  • Meinardus, Otto Friedrich August. Two Thousand Years of Coptic Christianity (2010)
  • Thomas, Martyn, ed. (2006). Copts in Egypt: A Christian Minority Under Siege : Papers Presented at the First International Coptic Symposium, Zurich, September 23–25, 2004. Vandenhoeck & Ruprecht. {{cite book}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  • Van Doorn-Harder, Nelly. "Finding a Platform: Studying the Copts in the 19th and 20th Centuries" International Journal of Middle East Studies (Aug 2010) 42#3 pp 479–482. Historiography

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]