Vladimir Vysotsky
Vladimir Semyonovich Vysotsky (25 Januari 1938 – 25 Julai 1980) alikuwa mwimbaji, mwanashairi na mwigizaji katika Umoja wa Kisovyeti. Hakukubaliwa na serikali ya siku zake lakini malipendwa sana na watu na hadi leo ana athiri kubwa juu ya wanasanii nchini Urusi.
Babake alikuwa mwanajeshi Mrusi wa Kiyahudi, mamake Mrusi. [1] Tangu utoto aliwashangaza watu wengine kwa uwezo wake kutunga shairi mara moja, kufanya maigizo na kuimba.
Aliimba tofauti na wote wengine wa siku zake na hakukubali kubanwa na mamlaka ya serikali juu ya utamaduni na sanaa. Aligusa pia mada ambazo hazikukubaliwa na mamlaka ya sanaa ingawa zilikuwa matatizo halisi katika jamii kama vile uhaini, chuki dhidi ya Wayahudi na ukahaba.
Nyimbo nyingi hazikupewa nafasi katika redio au kwenye rekodi za makampuni rasmi kwa hiyo wasikilizaji wake walirekodi wenyewe alipoimba na kusambaza nyimbo kati yao wenyewe kwa njia ya samisdat.
Alikuwa pia mwigizaji katika filamu nyingi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-08. Iliwekwa mnamo 2012-12-19.