Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Wakutu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wakutu ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Morogoro Vijijini, vijiji vya Ukutu, Kiburumo, Magogoni, Kiganira, Kibiro, Bwila, Kidunda na vinginevyo.

Wakutu hawatofautiani sana na Waluguru na Wazaramo, na kama wao ukoo unafuata upande wa mama, yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.

Pia lugha yao, ambayo ni Kikutu, haina tofauti kubwa na Kiluguru na Kizaramo.

Mwaka 1987 walikadiriwa kuwa 45,000.

Koo maarufu za Kikutu ni Ndago (ni miongoni mwa familia kubwa katika kabila la Kikutu: Mussa Ndago alikuwa na watoto 25, Omary Ndago 20 na Ramadhani Ndago watoto 15; jumla ina wajukuu 130) lakini pia Makinda na Mkuyu.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakutu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.