Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Uzushi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wazushi)

Uzushi ni hali ya kueneza habari zisizo na ukweli au habari za uongo kabisa. Mtu anayeeneza uzushi huwa na madhumuni ya kumdhalilisha mwingine, kumuharibia sifa yake na kadhalika.

Uzushi huweza kumfanya mtu aliyezushiwa jambo kuwa na hofu, kutojiamini, kujitenga na watu, kutokuwa na uhuru, kutofanya maamuzi sahihi.

Pia uzushi au uongo huweza kutumiwa na watu katika kueneza imani potofu, kuhimiza watu kufanya mabaya na kadhalika.

Uongo hutumiwa zaidi na wanasiasa katika kujitafutia kura kutoka kwa wananchi.

Kwa matumizi ya istilahi hii kuhusu mafundisho ya kidini, ona Uzushi wa kidini.