Zen
Zen ni jina la aina ya Ubuddha inayopatikana hasa nchini Japan na katika karne ya 20 imesambazwa katika nchi nyingi duniani. Ilianzishwa wakati wa karne ya 5 BK katika mkondo wa Ubuddha wa Mahayana nchini China ikaendelea ukua hasa Japan.
Mkazo wa Zen si mafundisho wala imani bali mazoezi hasa katika hali ya mazingatio kimya kwa lengo la kufikia hali ya mwangaza wa ndani.
Shairi ya kale inaonyesha mwelekeo wa Zen, na hasahasa mstari wa nne:[1]:
Mapokeo maalumu nje ya maandiko
bila kutegemea neno wala herufi
moja kwa moja kuonyesha moyo wa binadamu
kuona nafsi ya mwenyewe na kuwa Buddha
Jambo muhimu ni uhusiano kati ya mwalimu na mwanafunzi. Mwalimu ni mtu aliyeona mwangaza akikubali wajibu wa kuwafungulia wengine njia hii pia.
Kufuata njia ya mwangaza ni kazi ya Zazen. Zazen inamaanisha kuketi katika hali ya mazingatio kimya. Mwenyekutafuta mazingatio kimya anaketi chini, mguu mmoja juu ya mwingine. Uti wa mgongo haunyoki na mikono inakaa moja juu ya mwingine bila kuisukuma, ncha za vidole gumba hugusana kidogo. Macho yako wazi kiasi kwa kuangalia chini lakini bila kutazama kitu.
Roho inatazama hali ya wakati bila kutafakai kitu. Mwenye kufuata mazingatio kimya anaangalia pumzi yake na mwili wake, anatazama nafsi yake na fikra. Kwa njia hii anatarajia kuwa kimya kabisa na kufikia hali ya amani ya ndani.
Kurasa husika
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Heinrich Dumoulin: Geschichte des Zen-Buddhismus. Band I: Indien und China. S. 83 (Historia ya Ubuddha wa Zen)