Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Maana Quotes

Quotes tagged as "maana" Showing 1-11 of 11
Enock Maregesi
“Lakini damu na maji vina maana kubwa katika maisha yetu. Biblia inaeleza kuwa wakati Yesu Kristo akiwa msalabani alichomwa ubavu wake kwa mkuki, ikatoka damu na maji, ndipo zilipozaliwa sakramenti za kanisa. Aidha, tukio la askari wa Kirumi kumchoma Yesu na damu na maji kutoka lina maana nyingine kubwa katika maisha yetu. Hapo ndipo Ukristo ulipozaliwa; na ni kwa sababu hiyo mwanamke anapojifungua hutoa damu na maji kutokana na kupasuka kwa utando wa mfuko wa uzazi. Kutokana na hayo, Wakristo wanapoabudu msalaba wanaeleza umuhimu wa matukio na mafundisho waliyopata kupitia mateso aliyopata kiongozi wao na kuwa, msalaba ni chombo cha ukombozi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ina maana kwa sababu ya wanawake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ikiwa huna pesa na una mke na watoto kwa mfano, mke wako (wanawake walio wengi) hatakuona wa maana kwa sababu ya ustawi wa maisha ya familia yake. Ikiwa una mwanamke asiyekuwa na busara au hekima ya kutosha, au mwanamke ambaye akili zake zimefyatuka kidogo, atakusaliti kutafuta bwana au mtu mwenye maana. Kama huna pesa huna maana kwa mwanamke.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nilijifunza toka awali umuhimu wa kushindwa katika maisha ijapokuwa nilijitahidi sana, na nilipoendelea kushindwa niliweka nadhiri ya kufanya kitu kimoja kilicholeta maana zaidi katika maisha yangu nacho ni uandishi wa vitabu. Uandishi wa vitabu ndicho kitu pekee nilichokiweza zaidi kuliko vingine vyote na kuanzia hapo Mungu aliniweka huru. Nilijua mimi ni nani. Nilijua kwa nini nilizaliwa. Nilijifunza falsafa ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko nilivyoikuta – kwa sababu hata mimi nilikuwepo – na falsafa ya kushindwa si hiari. Maarifa hayo yakafanya niwe na heshima na upendo kwa watu wote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Fikiria kwanza maana ya kitu unachofikiria, halafu tenda. Fikiria kwanza maana ya kitu unachosema, halafu sema.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tafuta kitu cha kufanya katika maisha yako unachokiamini zaidi kuliko pesa, kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika kwa mfano, na ukishakipata kuwa kiongozi na mkarimu kwa wengine. Kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika inaweza kuwa ndiyo nafasi yako uliyopangiwa na Mungu uitumie kwa manufaa ya wengine, si kwa manufaa yako, nafasi za wengine zitatumika kwa manufaa yako. Kuna vitu vingi ambavyo mtu anaweza kufanya; chagua kimoja kinacholeta maana zaidi katika maisha yako na ukifanye hicho, kwa nguvu zako zote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Njia rahisi ya kujua maana ya ndoto zako ni kurekodi ndoto zako kila siku asubuhi, au kila unapoota, kwa angalau majuma mawili. Baada ya muda huo ndoto zako zitaanza kuleta maana. Lengo lake kubwa ni kukufanya ujitambue.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwa makini, nadhani, utapata maana ya ujumbe unaopewa na Roho Mtakatifu kwa wale wanaomwamini Mungu au ‘daemon’ (tofauti na ‘demon’) kwa wale wasiomwamini Mungu. Mimi, kwa mfano, huwa najali muda. Jicho langu likicheza au kiungo changu chochote cha mwili kikiuma ghafla na kuacha, au hata kisipoacha, jambo lolote ninalolifikiria muda huo ambapo jicho linacheza au kiungo changu cha mwili kinauma najua ni ujumbe kutoka kwa Mungu na una uhusiano na jambo hilo ninaloliwaza. Hivyo, kuanzia sekunde hiyo napaswa kuwa makini sana na jambo lolote ninalolifikiria.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mwenye hekima huzungumza kilicho na maana! Kinaweza kuwa kizuri au kibaya.”
Enock Maregesi