Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Ndoto Takatifu Quotes

Quotes tagged as "ndoto-takatifu" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Ndoto za wachawi ni tofauti kidogo na ndoto takatifu. Wachawi wanapokuwa hawahitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini wana hamu ya kuona wenzao wanafanya nini au wanasema nini, huwa wanalala ubavu mmoja upande wa kushoto kwa jina la mungu wao na la mashetani wote. Kisha wanatoa mvuke wa bluu midomoni mwao. Kupitia mvuke huo, kwa nguvu za Shetani na kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, wataona na watasikia kila kinachofanyika upande wa pili. Kile wanachotaka kukiona na kukisikia hujifunua katika ufahamu wao kama taswira au maono, kutoka katika akili isiyotambua, ya watu wakifanya au wakisema kitu. Kama wanataka kujua siri za watu wengine, hata wale ambao si wachawi, watazijua kupitia ndoto hizo; kwa sababu ya makubaliano ya wazi, si ya siri, waliyoingia na Shetani. Makubaliano hayo si ya lelemama; yaani yale ambayo hufanywa kwa kutoa kafara ya mnyama, au kufuru ya aina yoyote ile kwa Mwenyezi Mungu, au kwa kuabudu dini za kichawi. Lakini ni kwa sadaka halisi ya wao wenyewe ya mwili na roho kwa Shetani na kwa kufuru ya kuikana kabisa, imani ya Mwenyezi Mungu. Lakini hiyo ni kwa wale wanaotumia uchawi wa kishetani. Wale wanaotumia uchawi wa asili, kama vile kutumia risasi kumroga mtu kwa sababu risasi mungu wake ni sayari ya Zohali, au wale walioingia mkataba wa siri na Shetani, hawana uwezo wa kuota hivyo. Hivyo, si kila mchawi anaweza kuota ndoto za namna hiyo, ni kwa wale tu walioingia mkataba wa wazi na Shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini kuna ndoto takatifu na kuna ndoto za kishetani. Ndoto takatifu hutokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika, kama ambavyo usiku unavyokuwa kimya na kila kitu kimetulia, karibu na saa za alfajiri, ambapo mfumo wa usagaji chakula unakuwa umemaliza kazi yake. Kipindi hicho malaika wa Mungu hutufunulia siri kuhusu ulimwengu huu, ili kwamba tutakapoamka asubuhi tuwe na baadhi ya maarifa yaliyojificha ndani ya maandiko ya vitabu vitakatifu; kwa sababu malaika wa Mungu ndiye anayetawala ufahamu wetu, kama ambavyo Mungu anavyotawala hiari yetu, na kama ambavyo nyota zinavyotawala miili yetu. Lakini kwa wale waliokomaa kiimani malaika mwema anaweza kuwafunulia siri wakati wowote, haijalishi wamelala au wameamka. Kwa ajili ya ujanja wa Shetani ndiyo maana Mungu hutufunulia siri zake, ili tujihadhari naye.”
Enock Maregesi