Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Siku ya wapendanao

Siku ya wapendanao (kwa Kiingereza: Valentine's Day) ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka.

Mawaridi ni zawadi ya kawaida kwa mchumba wa kike, hasa siku hiyo.
Zawadi ya chokoleti maalumu kwa siku hiyo.
Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu mapendo

Moyo katika mapokeo ya Ulaya
ni mchoro unaowakilisha mapendo.
Vipengele Msingi
Mapendo kadiri ya sayansi
Mapendo kadiri ya utamaduni
Upendo (fadhila)
Upendo safi
Kihistoria
Mapendo ya kiuchumba
Mapendo ya kidini
Aina za hisia
Mapendo ya kiashiki
Mapendo ya kitaamuli
Mapendo ya kifamilia
Mapendo ya kimahaba
Tazama pia
Mafungamano ya binadamu
Jinsia
Tendo la ndoa
Maradhi ya zinaa
Siku ya wapendanao

Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma au Terni ambapo alikuwapo padri au askofu Valentinus ambaye akaja kuheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe hiyo.

Hadithi zilizosababisha sikukuu kuenea

hariri

Inasemekana kwamba Kaisari wakati huo alikuwa Claudius II: yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera). Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.

Valentinus alipinga jambo hili na hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuuawa.

Kuna hadithi nyingine ya kuwa akiwa gerezani Valentinus aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za kwanza za Valentine kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.

Mbali ya hadithi, askofu huyo alijulikana kwa miujiza yake. Huko Terni, mnamo 2011, ilipatikana mifupa ya Sabino e Serapia: mmoja alikuwa Mpagani akida wa jeshi la Roma, mwingine msichana Mkristo motomoto. Kwa ajili yake Sabino aliongokea Ukristo, lakini baada ya muda mfupi aligundua kwamba Serapia ni mgonjwa wa kifua kikuu. Ili asitengane naye, Sabino alimuomba Valentinus, naye alibariki ndoa yao na kuomba mapendo yao yadumu milele. Baadaye walifariki pamoja wamekumbatiana na ndivyo mifupa yao inavyopatikana hadi leo.

Toka hapo Valentine anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani.

Kuna matukio kadha wa kadha kutokana na historia ya siku hiyo ikiwemo kufungwa jela kwa askofu Mt. Valentinus wa Roma kutokana na kuwatesa baadhi ya Wakristo katika Dola la Roma mnamo karne ya 3.

Kulingana na tamaduni za kale, Askofu huyo alimponya mtoto kipofu wa mfungwa mwenzake. Ndipo mara nyingi matendo yake yanahusishwa na kitendo kikuu cha upendo: kuna baadhi ya historia zinasema kuwa askofu huyo alimtumia barua mtoto wa yule mfungwa mwenzake aliyemponya upofu, na barua hiyo ilikuwa ni katika hali ya kumuaga akiendea kutimiza kifungo chake na adhabu ya kunyongwa. Historia zinazidi kusema kuwa mwishoni mwa barua hiyo kulikuwa kumesainiwa kwa maneno yaliyosema "Valentinus wako".

Lakini pia baadhi ya tamaduni za watu zilizidi kusema kuwa askofu huyo aliwafungisha ndoa wanajeshi wawili ambao walikuwa wamekatazwa kufunga ndoa.

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siku ya wapendanao kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.