Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Makala hii inahusu mtazamo wa mtu. Kuhusu matokeo ya kimwili ona unene wa kupindukia, ulevi

Sehemu inayohusu ulafi katika mchoro wa Hieronymus Bosch kuhusu vilema vikuu saba na vikomo vinne vya binadamu.
Vilema vikuu

Ulafi (pamoja na ulevi) ni hamu isiyoratibiwa ya kula (na kunywa).

Tabia hiyo ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu.

Inakadiriwa kuwa siku hizi mtu 1 kati ya 3 anakula kuliko mwili wake unavyohitaji, na hivyo anasababisha maradhi mbalimbali yampate.

Upande wa maadili unahesabiwa kuwa dhambi, tena kimojawapo kati ya vilema vikuu, ambavyo katika mapokeo ya Wakristo mbalimbali ni mizizi ya dhambi nyingine, hata kubwa zaidi.