Nikotini : Tofauti kati ya masahihisho
d roboti Nyongeza: hr:Nikotin Badiliko: id:Nikotina, sr:Никотин |
mbegu-kemia |
||
Mstari 41: | Mstari 41: | ||
[[Category:madawa]] |
[[Category:madawa]] |
||
{{ |
{{mbegu-kemia}} |
||
[[ar:نيكوتين]] |
[[ar:نيكوتين]] |
Pitio la 15:10, 18 Juni 2009
Nikotini ni dutu ya alkaloidi katika mimea mbalimbali hasa tumbaku ambayo ni dawa linaloathiri neva za mwanadamu. Matumizi yake ni hasa katika sigara, lakini pia katika kemikali na madawa.
Kuanzia kiasi fulani ni sumu kali, kwa viwango vidogo inaamsha neva za watu. Hatari yake kwa mwanadamu ni hasa uzoefu unaotokea na kuwa haraka uraibu unaotawala mwili na roho kwa hamu ya kurudia matumizi ya nikotini. Katika sifa hii inafanana na madawa ya kulevya hata kama kiwango cha kumwamsha mtu haufikii kwenye hali ya ulevi wa namna yoyote.
Matokeo ya nikotini yanayotafutwa na watu
Matokeo ya kimwili ya nikotino kwa kiwango kidogo ni kuharakisha pigo la moyo na kupandisha kanieneo ya damu. Sifa hii inatafutwa na watu wakisema matumizi ya tumbaku husaidia kuondoa au kupunguza uchovu na kuongeza uamsho wa bongo. Lakini uamsho huu haudumu muda mrefu na mtu anapaswa kuongeza nikotini mara nyingi kwa kuvuta sigara nyingine.
Hasara na hatari zake
Hatari hasa ya dawa lenyewe ni uraibu ya hatari ya kutawaliwa nayo.
Sumu ya neva
Kwa viwango kikubwa zaidi hatari zake kama sumu ya neva ni muhimu. Kiwango cha miligramu moja ya nikotini kwa kilogramu moja ya uzani wa mtu kinatosha kumwua mtu. Yaani mtu mwenye uzani wa 70 kg hufariki akiingiza miligramu 70 mwilini. Hapa ni kwa mfano hatari ya watoto wadogo kula sigara bila kujijua: sigara moja huwa na miligramu 10 za nikotini. Mvutaji anaingiza sehemu yake tu kwa njia ya moshi lakini mlaji anapata yote na mtu mdogo huwa hatarini kabisa.
Nikotini ni kati ya sumu kali kabisa hivyo imetumiwa kama dawa la wadudu kwa sababu mimea haina matatizo naye ni wanyama tu. Lakini nchi nyingi zimepiga matumizi haya marufuku kutokana na hatari kwa watu wanaotumia dawa au wanaoishi katika mazingira ambako inatumiwa.
Sumu katika moshi ya sigara
Hasara za nikotini katika sigara zinaenda sambamba na kemikali zinazokuja pamoja nayo katika sigara kama njia kuu ya kutumia nikotini. Hapa wataalamu hawana uhakika kiasi gani magonjwa yanayoonekana katiy a wavutaji husababishwa na nikotini hasa au na nikotini pamoja na kemikali nyingine ndani ya moshi.
Hasara zilizotazamiwa ni kama vile:
- hamu ya kula inapungua
- asidi inaongezeka tumboni
- maumivu ya kichwa
- mishipa ya damu hujikaza; ianonekana kuna uhusiano na mishipa membama kati ya wavutajiwa miaka mingi
- hii inaongeza hatari ya magonjwa ya moyo
- inaogeza hatari ya thrombini yaani kuzibwa kwa mishipa ya damu
- viungo vya mwili vilivyo mbali na moyo havipokei damu na lishe ya kutosha; hapa ni sababu ya kuoza kwa miguu ya wavuta tumbaku.
- vidonda hupoa polepole
- nguvu ya kuzaa kwa wanaume hupungua
Jina
Jina la dawa latokana jina la kitaalamu la tumbaku "Nicotiana tabacum" na hili lilitokea na Jean Nicot aliyekuwa balozi wa Ufaransa nchini Ureno. Alijipatia mbegu za tumbako wakati mmea huu ulikuwa umeingia kutoka Amerika akazituma Paris kwa utafiti.
Dawa la nikotini ndani ya majani ya mmea lilibuniwa 1828 na wanakemia Wajerumani.
-
Muundo wa kikemia wa nikotini
-
Molekuli ya nikotini
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nikotini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |