Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Waborana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waborana

Mtu mwenye asili ya Kiborana akipiga kura katika kituo cha upigaji kura Marsabit, Kenya.
Maeneo yenye Idadi ya Watu yenye Maana
Ethiopia, Kenya

Waborana Oromo (ambao pia huitwa Boran) ni kabila lipatikanalo Kusini mwa Ethiopia, Oromia na Kaskazini mwa Kenya[1] ambao wanajulikana kuwa wafugaji. Wao ni kundi dogo la Waoromo[2]. Wanawakilisha nusu ya makundi mawili ya Waoromo asili, nusu nyingine ikiwa Wabarentu. Takribani watu milioni 7 wanajitambulisha kama jamii ya Waborana.

Waoromo wa Kaskazini mwa Kenya waliingia eneo hilo mara ya kwanza kutoka Kusini mwa Ethiopia wakati wa uhamiaji mkubwa wa Karne ya 10. Walitawanyika kuwa Waborana wafuga ng'ombe na wafuga ngamia, Wagabra na Wasakuye[3].

Waborana huzungumza Kiborana (au afaani Boraana), ambayo ni mojawapo ya Lugha za Kikushi ambayo pia ni mojawapo ya makundi makubwa ya Lugha za Kiafrika-Kiasia.

Kalenda ya Kiborana

[hariri | hariri chanzo]

Inaaminika kuwa Waborana wana Kalenda yao waliyoitunga karibu miaka ya 300 KK. Kalenda yao hutegemea matukio ya anga ya mwezi pamoja na Nyota Saba.

Miezi ya Kiborana (Mizunguko ya miezi na nyota) ni:

  • Bittottessa (iangulum),
  • Camsa (Pleiades),
  • Bufa (Aldebarran),
  • Waxabajjii (Belletrix),
  • Obora Gudda (Orion-Saiph ikiwa kati),
  • Obora Dikka (Sirius),
  • Birra (Mwezi mzima),
  • Cikawa (gibbous moon),
  • Sadasaa (Nusu-mwezi),
  • Abrasa (Kipande kikubwa cha mwezi),
  • Ammaji (Kipande cha wastani), na
  • Gurrandala (Kipande kidogo)[4].

Matabaka madogo

[hariri | hariri chanzo]

Waoromo wanajumuisha makundi mawili muhimu, ambayo hugawanyika katika koo nyingi za kifamilia. Kutoka Magharibi kuelekea Mashariki na Kaskazini kuelekea Kusini, matabaka hayo ni:

Kuna vikundi vingine vingi pia.

  1. Ethnologue;Ethnologue
  2. Aguilar, Mario. "The Eagle as Messenger, Pilgrim and Voice: Divinatory Processes among the Waso Boorana of Kenya". Journal of Religion in Africa, Vol. 26, Fasc. 1 (Feb., 1996), pp. 56-72. Iliwekwa mnamo 2007-10-27.
  3. Elliot M. Fratkin, Eric Abella Roth, As Pastoralists Settle, (Springer: 2005), p.39
  4. Lawrence R. Doyle, The Borana Calendar REINTERPRETED Archived 29 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.

Kusoma zaidi

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waborana kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.