Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Ellen DeGeneres

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ellen DeGeneres

Ellen DeGeneres, mnamo 2011
Amezaliwa Ellen Lee DeGeneres
26 Januari 1958 (1958-01-26) (umri 66)
Metairie, Louisiana, Marekani
Kazi yake Mchekeshaji
Miaka ya kazi 1978-hadi leo
Ndoa Portia de Rossi (2008-hadi leo)

Ellen Lee DeGeneres (amezaliwa 26 Januari 1958) ni mwigizaji wa filamu na mchekeshaji kutoka nchini Marekani. Maarufu kwa kipindi chake cha mazungumzo kinachokwenda kwa jina la Ellen Show, ni mama wa kwanza katika tasnia ya vipindi vya mazungumzo kujitokeza hadharani na kusema kwamba yeye anapenda mahusiano ya jinsia moja. Hatua hii ilipelekea kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa anaishi na baba yake mzazi kwa kuhofia kuambukiza tabia hiyo mbaya kwa ndugu zake wa kike wengine wawili waliozaliwa baba mmoja lakini mama tofauti. Wengi walihisi huenda mama wa kufikia alitia fitina kati yake na baba yake ili aondoke, jambo ambalo lilimuumiza Ellen lakini hatimaye aliyamaliza hayo.[1] [2]

Kwa mara ya kwanza aliuonesha umma wa watu wa Marekani kwamba yeye ni mpenzi wa mahusiano ya jinsia moja katika mfululizo wa TV wa Ellen uliokuwa unarushwa na TV ya ABC katika kisa maarufu "The Puppy Episode" kilichorushwa hewani tarehe 30 Aprili 1997. Kisa hicho kinamuelezea Ellen Morgan ana mahusiano na mwanamke mwenzake ambaye wakati huo alikuwa Laura Dern; kwa pamoja walipata tabu sana katika kazi zao za uigizaji, kazi zilipotea na wakaanza upya. Walitengwa na watu wengi, makundi mbalimbali wanaopinga mahusiano ya jinsia moja. Ilichukua muda sana hadi Ellen na mwenzake kurudi tena katika soko. Mwezi wa Agosti 2008, baada ya sheria ya kukinga ndoa za jinsia moja kuondolewa jijini Los Angeles, Ellen na Portia walioana rasmi kuwa mke na mke.[3]

Mbali na vipindi vya TV na kadhalika, Ellen vilevile ni mwandishi wa vitabu mbalimbali, kama vile:

  • DeGeneres, Ellen (1995). My Point...And I Do Have One. New York: Bantam Books. ISBN 0-553-09955-8.
  • DeGeneres, Ellen (2003). The Funny Thing Is... New York: Simon & Schuster. ISBN 0-7432-4761-2.
  • DeGeneres, Ellen (2011). Seriously...I'm Kidding. New York: Grand Central Publishing. ISBN 0-446-58502-5.
  • DeGeneres, Ellen (2015). Home. Grand Central Life & Style. ISBN 1455533564.
  1. News and sexuality : media portraits of diversity. Castañeda, Laura, 1963-, Campbell, Shannon B., Casta๑eda, Laura, 1963-. Thousand Oaks, Calif.: Sage Publications. 2006. ISBN 1412909988. OCLC 59881923.{{cite book}}: CS1 maint: others (link)
  2. Steven., Capsuto, (2000). Alternate channels : the uncensored story of gay and lesbian images on radio and television (tol. la 1st). New York, NY: Ballantine Books. ISBN 0345412435. OCLC 44596808.{{cite book}}: CS1 maint: extra punctuation (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. "Ellen and Portia's Love Story", Us Weekly (kwa American English), 2012-01-26, iliwekwa mnamo 2018-09-30

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ellen DeGeneres kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.