Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Hamburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Hamburg.






Hamburg

Bendera

Nembo
Hamburg is located in Ujerumani
Hamburg
Hamburg

Mahali pa mji wa Hamburg katika Ujerumani

Majiranukta: 53°33′55″N 10°00′05″E / 53.56528°N 10.00139°E / 53.56528; 10.00139
Nchi Ujerumani
Jimbo Hamburg
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 1,769,117
Tovuti:  www.hamburg.de
Picha ya ndege ya bandari ya Hamburg
Makontena huondelewa hapa kwenye meli

Hamburg ni mji mkubwa wa Ujerumani ya Kaskazini. Ni mji mkubwa wa pili nchini baada ya mji mkuu Berlin. Ina bandari kubwa na ni kitovu cha biashara ya nje. Idadi ya wakazi ni 1,744,215.

Hamburg ni dola-mji ikiwa ni moja ya majimbo 16 ya kujitawala ya Ujerumani. Jina rasmi ni „Mji Huru na Mji wa Hanse wa Hamburg“. Hanse ilikuwa shirikisho la kimataifa la miji ya biashara iliyojitawala zamani za Karne za kati. Kwa muda mrefu wa historia yake Hamburg ilikuwa kama nchi ndogo ya kujitegema hadi kujiunga na Dola la Ujerumani mwaka 1871.

Hamburg iko kando ya mto Elbe unaopanuka baada ya kupita mji kuwa na mdomo mpana sana kabla ya kuishia Bahari ya Kaskazini. Meli kubwa zinaweza kuingia mtoni ambako ni salama kabisa na dhoruba za baharini.

Wafanyabiashara wa Hamburg waliwahi kuwa na biashara na nchi za nje kwa jahazi na meli zao tangu karne nyingi. Hata mawasiliano kati ya Afrika na Ujerumani yalipitia hasa Hamburg na mji jirani wa Bremen.

Leo Hamburg pamoja na mazingira yake ni kitovu cha biashara, uchumi na utamaduni wa Ujerumani ya Kaskazini. Kuna viwanda vya ndege za Airbus, viwanda vyaa bidhaa za matumizi ya kila siku, magati, bandari ya 4331 ha iliyoshughulika makontena milioni 8.1 katika mwaka 2005. Hamburg ni mji ambako magazeti mengi ya kitaifa yanatolewa.

Usafiri wa jiji huendeshwa na Ushirika wa Usafiri wa Hamburg HVV.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]


 
Majimbo ya Ujerumani
Baden-WürttembergBavaria (Bayern)BerlinBrandenburgBremenHamburgHesse (Hessen)Mecklenburg-Pomerini Magharibi (Mecklenburg-Vorpommern)Saksonia Chini (Niedersachsen)Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)Saar (Saarland)Saksonia (Sachsen)Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)Schleswig-HolsteinThuringia (Thüringen)
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hamburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.