Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Hathor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Hathor akibeba duara ya Jua kati ya pembe (Jumba la kumbukumbu la Luxor)

Hathor alikuwa mmoja wa miungu katika dini ya Misri ya Kale. Alikuwa mungu wa kike aliyepewa nafasi mbalimbali katika imani ya watu. Wakati wa nasaba ya kwanza aliabudiwa kwa umbo la ng'ombe. Baadaye aliaminiwa kuhusika na anga akaabudiwa kama mama wa miungu mingine, hasa mungu Ra aliyekuwa Jua. Alikusika pia na mapenzi, amani, uzuri, sanaa na muziki.

Mwonekano

[hariri | hariri chanzo]

Hathor alioneshwa katika maumbo manne tofauti. Kwa sura ya kibinadamu, Hathor alikuwa na kichwa cha ng'ombe na pembe mbili za ng'ombe, kwa sababu ng'ombe walikuwa wanyama wenye thamani kubwa.

Katika moja ya maumbo yake ya kinyama, alikuwa ng'ombe mwenye ankh. Ankh ilikuwa ishara ya uhai.

Umbo lingine la kinyama la Hathor lilikuwa simba mkali.

Ishara ya Hathor ilikuwa ng'ombe anayebeba duara ya Jua kati ya pembe zake. Wamisri waliwaza kwamba Hathor anamzaa Ra, mungu wa Jua, kila asubuhi akiendelea kumbeba angani kati ya pembe zake.