Muziki
Muziki ni mpangilio wa sauti ili kuunda mseto wa umbo, utangamano, melodi, mdundo, au vilevile mbinu elezi. Muziki kwa ujumla unakubaliwa kuwa utamaduni wa ki-ulimwengu na hupatikana katika jamii zote za wanadamu.
Ufafanuzi wa muziki hutofautiana sana kifalsafa na kimbinu. Ingawa wasomi wanakubali kwamba muziki unafafanuliwa na vipengele maalum, hakuna makubaliano kuhusu uhakika wa vipengele hivi. Mara nyingi, muziki hutambulishwa kama mbinu ainati ya kuwasilisha ubunifu. [1]
Shughuli mbalimbali huhusika katika uundaji wa muziki, na mara nyingi hugawanywa katika kategoria za utunzi, ubunifu tendi na uigizaji. Muziki unaweza kuimbwa kwa kutumia ala mbalimbali za muziki, ikiwemo sauti ya binadamu. Inaweza pia kutungwa, kupangwa, au kuchezwa kifundi au kielektroniki, kama vile kisanduku muziki, paipu bareli, au programu dijitali kwenye kompyuta.
Muziki ni aina ya sanaa inayotumia sauti mbalimbali: za kibinadamu na za ala za muziki, ama kwa pamoja au kila moja pekee.
Asili ya neno iko katika lugha ya Kigiriki ambamo huitwa μουσική (mousikee).
Baadhi ya sifa za muziki ni uzito wa sauti (pitch) na wizani au mahadhi (rhythm).
Aina ya muziki inayopatikana kote duniani ni nyimbo ambazo ni maneno yanayotolewa kwa sauti na mahadhi fulani mara nyingi pamoja na ala za muziki. Kwa wanaorekodi sauti, wao huenda kwa studio kurekodi na huchukuliwa kwa kinasasauti kilichoambatanishwa na tarakilishi na kudhibitiwa na kompresa.
Wanamuziki maarufu wa Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Ali Kiba, Diamond Platnumz, Ay, Ben Paul, Juma Jux, Maua Sama, Vanessa Mdee, Mwana FA, Joh Makini, Fid Q, Nandy, Bilnass, Belle 9, Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Queen Darling, Ibrah, Young Lunya, Baraka Da Prince, Lady Jay Dee, Anton Bruno, Baba Levo, Tanzania.
Wanamuziki maarufu wa Ulaya
[hariri | hariri chanzo]- Dua Lipa, Little Mix, Coldplay, One Direction, Ellie Goulding, Tinie Tempah, Dizzee Rascal, Skepta, Charli XCX, Calvin Harris, Stormzy, Jax Jones (Ufalme wa Muungano)
- Felix Jaehn, Nena, Kay One, Alex C, Alle Farben, Eko Fresh, Bausa, Dagi Bee, Capital Bra, Robin Schulz, Bushido, Namika, Scooter, Rammstein, Kraftwerk, Zedd, 187 Strassenbande, Marc Engelhard, Bonez MC, Gzuz (Ujerumani)
- Cleo, Doda, Sitek, Natalia Nykiel, Ewelina Lisowska, Sokół, Tede, Donguralesko, Margaret, Donatan, Gromee, Sławomir, Zespol Akcent, Taconafide, C-BooL (Poland)
- Timati, Feduk, T.A.T.u., Max Korzh, Gamora, Oxxxymiron, Serebro, Rompasso, Gorky Park, Filatov & Karas, Vremya i Steklo, Allj, Algie & Kravtsov (Urusi)
- Álvaro Soler, Enrique Iglesias, Rels B (Hispania)
- Black M, Willy William, Stromae, Maître Gims, Indila, Kendji Girac, Daft Punk, Imany, David Guetta, Soprano, Martin Solveig (Ufaransa)
- Andrea Bocelli, Gigi D'Agostino, Ghali, Francesco Gabbani, J-AX, Alex Gaudino, Fedez, Guè Pequeno, Benny Benassi, Marracash, Sfera Ebbasta, Tacabro (Italia)
- Inna, Alexandra Stan, Elena, Dan Balan, G Girls, Akcent, Sandu Ciorba, Morandi (mwanamuziki) (Romania)
- Ektor, Rest, Krystof, Slza, Atmo Music, Helena Vondrackova (Ucheki)
- Kontrafakt, Celeste Buckingham, Rytmus, Majk Spirit (Slovakia)
- Ruslana, Jamala, Pianoboy, Alekseev, Monatik, VovaZIL'Vova, TNMK, Seryoga, Yarmak (Ukraine)
- ABBA, Zara Larsson, Swedish House Mafia, Danny Saucedo, Basshunter, Loreen, Galantis, Cherrie, Thrife, DJ Black Moose, Lykke Li (Uswidi)
- Kygo, Alan Walker, Sigrid, Marcus & Martinus, Madcon, Jesper Jenset (Norwei)
- The Rasmus, Alma, Nightwish, Lordi (Ufini)
- Tiësto, Afrojack, Hardwell, Martin Garrix, Armin van Buuren, Nicky Romero, Sbmg, Boef, Laidback Luke, Oliver Heldens, Natalie La Rose (Uholanzi)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Gzuz and Bonez MC
-
Zara Larsson
-
Tiesto
-
Inna
-
Sławomir
-
Timati
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hoad, T. F., ed. (2003). "music". The Concise Oxford Dictionary of English Etymology. . https://www.oxfordreference.com/view/10.1093/acref/9780192830982.001.0001/acref-9780192830982-e-9933.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- BBC Blast Music Ukurasa wa kujifunza mambo mbalimbali ya muziki kwa wenye umri wa miaka 13=19.
- The Virginia Tech Multimedia Music Dictionary
- The Music-Web Music Encyclopedia kwa ajili ya wanamuziki, watunzi na wapenda muziki.
- Dolmetsch free online music dictionary Kamusi ya muziki
- Musical Terms – Faharasa ya muziki toka Naxos
- "On Hermeneutical Ethics and Education: Bach als Erzieher", Makala ya Profesa Prof. Miguel Ángel Quintana Paz kuhusu historia ya maoni tofauti kuhusu muziki wa nchi za Magharibi toka enzi za Ugiriki ya Zamani hadi hivi sasa.
- Makala kuhusu muziki toka Bloomingdale School of Music Ilihifadhiwa 29 Mei 2016 kwenye Wayback Machine.
- Arts and Music Uplifting Society towards Transformation and Tolerance Ilihifadhiwa 17 Januari 2020 kwenye Wayback Machine. Makala kuhusu nguvu za muziki kwenye nyanja za mawasiliano, elimu na tiba.
- Scientific American, Musical Chills Related to Brain Dopamine Release
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muziki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |