Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Huduma ya kwanza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msalaba kati ya rangi ya kijani kibichi ni alama ya huduma ya kwanza kwa mfano kwenye kisanduku cha huduma ya kwanza chenye plasta na bendeji inayowekwa katika magari kwa nafasi za ajali.

Huduma ya kwanza inamaanisha huduma au msaada unatolewa kwa mtu anayekabiliwa na ugonjwa au madhara ya ghafla wakati daktari hayupo karibu na kabla hajapelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Kwa mfano huduma ya kwanza inatolewa wakati mtu anapopatikana baada ya ajali amejeruhiwa kwa shabaha ya kutunza uhai wake hadi mganga atakapopatikana au mjeruhiwa atakapoweza kufikishwa hospitalini.

Shabaha nyingine ni kuzuia kuongezeka kwa madhara kwa mfano kwa kumwondoa sehemu yenye hatari kama moto, hatari ya mlipuko au mahali penye hatari kwake binafsi.

Huduma ya kwanza inaweza pia kutaja misaada midogo kama kumpatia mtu plasta ya kufunika kidonda kisicho kikubwa.

Katika nchi nyingi mtu yeyote anayefanya mtihani wa liseni ya kuendeshea gari anahitaji kuonyesha ya kwamba alihudhuria masomo kadhaa alipopata elimu ya msingi kuhusu huduma ya kwanza.

Umuhimu wa huduma ya kwanza

[hariri | hariri chanzo]
  • Kuokoa maisha ya mgonjwa.
  • Kupunguza maumivu kwa mgonjwa.
  • Kuleta matumaini kwa mgonjwa.
  • Unasaidia kupunguza kidonda.

Vidokezo vya msingi

[hariri | hariri chanzo]

Tathmini ya kwanza

[hariri | hariri chanzo]
  • Dhibiti kuvuja damu; Chunguza njia za hewa za mtu aliyeumia, Kupumua kwake na Mzunguko wa damu; Tulia

Kumbuka usafi wa kimsingi.

  • Nawa mikono yako kabisa ili kupunguza kuenea kwa maambukizi.
  • Ikiwezekana, tumia mavazi ya kujikinga.
  • Hakikisha majeraha ni safi nama kavu, badilisha bandeji mara kwa mara ili kuzuia maambukizi.
  • Ikiwa maji yanapatikana, hakikisha mgonjwa ana maji ya kutosha mwilini.
  • Usimpe mgonjwa viowevu ikiwa amepoteza fahamu, hawezi kumeza chochote au amejeruhiwa vibaya.
  • Usaidizi wa Kimsingi wa Maisha/Ufufuzi Kupitia Mishipa ya Moyo ni mibano 30 ya kifua kwa kila mipumuo yako 2 ya uokoaji.
  • Ikiwa uso umejeruhiwa, fanya mibano pekee.
  • Jaribu uwezavyo usishtuke
  • Vuta pumzi nyingi...kupitia puani, kisha uzitoe polepole kupitia midomo iliyofunguka kidogo ili uweze kutulia na *kupunguza kiwango cha midundo ya moyo.

Kutibu majeraha ya moto

[hariri | hariri chanzo]
  • Poza majeraha ya moto kwa maji.
  • Majeraha mengi ya kuchomwa na kemikali hupozwa kwa maji.
  • Yafunge majeraha ya moto ili kuzuia maambukizi.
  • Mfuko safi wa plastiki unaweza kutumika kufunika majerahna ili kuzuia maambukizi.
  • Majeraha ya moto kwenye njia za hewa, viungo muhimu, kichwa, kiwiliwili, koo na kiungo chote ni majeraha hatari.
  • Majeraha kwenye njia za hewa yanaweza kutulizwa kwa kidonge cha barafu.

Kusitisha kuvuja damu

[hariri | hariri chanzo]
  • Sitisha kuvuja damu kwa: shinikizo la moja kwa moja; kuinua ikiwa mifupa haijavunjika; au shinikizo lisilo la moja kwa moja.
  • Shinikizo lisilo la moja kwa moja kwenye miguu: tumia vidole kuweka shinikizo katika sehemu ya ndani ya eneo la juu la mkono.
  • Jijaribie mwenyewe ili kupata eneo linalovuja damu, mkono wako utapata hisia tofauti.
  • Shinikizo lisilo la moja kwa moja kwenye miguu ili kusitisha kuvuja damu.
  • Tia shinikizo ukitumia ngumi, goti au mguu kwenye vifaa laini kwenye kinena.

Majeraha ya kichwa

[hariri | hariri chanzo]
  • Majeraha ya Kichwa-Mtu mwenye fahamu.
  • Inua kichwa na mabega.
  • Tathmini kiwango cha kupumua na midundo ya moyo.
  • Usimwache mtu mwenye jeraha la kichwa bila kumshughulikia.
  • Tathmini kasi ya kupumua na midundo ya moyo.
  • Jeraha la Kichwa – Ikiwa viwango vya kupumua na midundo ya moyo itashuka chini ya kawaida, na kuzidi kupungua, basi kuna jeraha hatari.
  • Jeraha la Kichwa – Kutapika kunaashiria jeraha hatari.

Kutathmini kupumua

[hariri | hariri chanzo]
  • Ili kupima kasi ya kupumua, mlaze mgonjwa chini.
  • Kisha hesabu ni mara ngapi kifua chake kinainuka kwa dakika moja.
  • Hiki ndicho kiwango cha kupumua.
  • Ugumu wa kupumua-mtu mwenye fahamu.
  • Inua kichwa/mabega; ikiwa ni jeraha la kifua, mwegemeze mgonjwa kwenye upande alioumia ili kulikinga pafu lisilojeruhiwa.

Viwango vya kawaida vya kupumua vya mtu aliyetulia kulingana na miaka

[hariri | hariri chanzo]
  • Kiwango tulivu cha kawaida cha kupumua cha mtoto mzawa– mipumuo 44 kila dakika
  • Kiwango tulivu cha kawaida cha kupumua cha mtoto mchanga– mipumuo 20 hadi 40 kila dakika.
  • Kiwango tulivu cha kawaida cha kupumua cha watoto wasioenda shule– mipumuo 20 hadi 30 kila dakika.
  • Kiwango tulivu cha kawaida cha kupumua cha watoto wakubwa– mipumuo 16 hadi 25 kila dakika.
  • Kiwango tulivu cha kawaida cha kupumua cha watu wazima– mipumuo 14 hadi 18 kila dakika.
  • Kiwango tulivu cha kawaida cha kupumua cha watu wazee– mipumuo 19 hadi 26 kila dakika.

Matibabu ya vidonda

[hariri | hariri chanzo]
  • Tengeneza vifaa vya kufungia kidonda kutokana na vitambaa safi.
  • Badilisha vifaa hivi mara kwa mara.
  • Chumvi na maji yanaweza kutumika kusafisha vidonda.
  • Aidini inaweza kutumika kusafisha vidonda lakini LAZIMA ichanganywe na maji.
  • Ili kujaribu, unapaswa kuweza kunywa kiowevu hiki bila kufunga mdomo.
  • Tepu inaweza kutumika kufunga vidonda vikubwa kama mshono wa kidonda unavyofunga.
  • Usijaribu kufunga kidonda kilichoachwa wazi kwa zaidi ya saa 6 – hii hutatiza uponaji.
  • Kifunike kidonda tu ili kuzuia maambukizi.

Majeraha ya kifua

[hariri | hariri chanzo]
  • Majeraha ya Kifua-mtu asiye na fahamu.
  • Mlaze kwa upande ulioumia = pafu lisilojeruhiwa huwa upande wa juu na hufanya kazi vizuri.
  • Huenda kukawa na kuvuja damu kwa ndani.
  • Fuatilia ili kutambua ishara za mshtuko kama vile midundo ya moyo iliyoongezeka, ubaridi, ngozi iliyokwajuka.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Huduma ya kwanza kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.