Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Itale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Miamba mikubwa ya itale inakaa kama pandikizi la kobe

Itale (pia: matale; kwa ing. granite) ni mwamba mgumu wenye asili ya kivolkeno.

Imetokea pale ambapo magma imepoa na kuganda. Ndani ya magma kuna madini mbalimbali na mengine yalianza kuganda mapema kuwa fuwele wakati wa kupoa zinazoonekana kama punjepunje ndani ya itale.

Itale ni sehemu kubwa ya ganda la dunia. Inatokea ndani ya ganda lakini kutokana na mwendo wa gandunia ndani ya ganda sehemu kubwa zimesukumwa juu na kuwa milima ya itale au pandikizi ya miamba tu.

Itale ni jiwe bora kwa ujenzi. Ni ngumu sana, hivyo kuta za itale ni imara kabisa. Kama itale inakatwa, kusuguliwa na kung'arishwa inapata uso wa kupendeza unaofaa kwa mapambo ya ukuta, sakafu au meza za kazi.

Kwa uchongaji sanamu ni jiwe gumu sana linaloleta matokeo ya kudumu.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Itale kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.