Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Metali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chuma ya moto ikifuliwa na mhunzi.

Metali (kutoka Kiingereza metal) ni kundi la elementi zenye tabia za pamoja kama vile

  • zinapitisha umeme kwa urahisi
  • zinapitisha joto
  • zinang'aa
  • ni wayaikaji (zinaweza kubabatizwa kuwa wembamba kama waya au kupinduliwa kabla ya kuvunjika)

Kikemia tabia hizo zote zinatokana na muungo metali ya elementi hizo. Kinyume chake simetali kwa kawaida ni kechu kama mangu, hazing'ai na zinahami (hazipitishi umeme).

Idadi kubwa ya elementi katika mfumo radidia huhesabiwa kati ya metali. Kuna pia elementi zinazoonyesha tabia za kati ya metali na simetali kama vile metaloidi au nusumetali.

Mifano ya metali ni

Historia ya matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Metali zimetumiwa na binadamu kwa vyombo vyao tangu zamani. Mwanzoni watu walitumia mawe tu kwa vifaa vingi, lakini baadaye walitambua faida ya metali. Hapo ilikuwa lazima kujifunza jinsi ya kutoa metali yenyewe katika hali ya oksidi au michanganyiko ya matapo jinsi zinavyotokea kwa kawaida.

Metali za kwanza zilizotumiwa ni dhahabu na shaba zinazoweza kupatikana kama metali tupu na safi. Ziko laini, hivyo zinaweza kupewa umbo kwa kupigwa kwa nyundo ya jiwe. Kuna mifano ya mapambo ya kale sana.

Katika Asia na Ulaya shaba ilikuwa metali ya kwanza iliyotumiwa na watu. Baadaye waliiyeyusha na kukoroga pamoja na stani kuwa aloi ya bronzi ambayo ni ngumu zaidi.

Takriban mnamo 1200 KK watu walianza kutumia chuma. Maarifa hayo yalienea katika pande nyingi za dunia.

Katika Afrika watu walianza kutumia moja kwa moja chuma jinsi inavyoonekana kutokana na utafiti wa akiolojia katika Nigeria.

Mgodi mkubwa wa shaba katika New Mexico (Marekani).

Kupatikana kwa metali

[hariri | hariri chanzo]

Metali zinapatikana mara nyingi ndani ya miamba mbalimbali kama mtapo. Kunatokea pia ya kwamba zinapatikana kama metali tupu. Lakini njia ya kawaida ni kuvunja mwamba wenye mtapo ndani yake na kutoa metali kwa njia ya joto au kwa kutumia kemikali.

Mahali pa kuchimba metali huitwa migodi. Mara nyingi ni lazima kuchimba chini ya uso wa ardhi ili kupata mtapo.

Vitu vingi vya kimetali ni mchanganyiko au aloi za metali pamoja na metali nyingi au pia simetali. Aloi zinazotumiwa zaidi ni:

Tabia ya kimetali za nyota

[hariri | hariri chanzo]

Katika fani ya astronomia jina "metali" hutumiwa kwa maana tofauti. Hapa nyota ina tabia ya kimetali (metallicity) kama ndani yake ina elementi ambazo ni nzito kuliko hidrojeni na heli. Wakati mwingine wanaangalia tu elementi nzito kuliko kaboni katika makadirio ya "tabia ya kimetali".

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.