Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Mto Madeira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Madeira (Rio Madeira)
Beseni ya Amazonas pamoja na Mto Madeira
Chanzo kuungana kwa mito Madre de Dios na Mamoré
Mdomo Mto Amazonas
Nchi Bolivia, Brazil
Urefu km 3,380
Kimo cha chanzo m 180
Tawimito upande wa kulia Mito ya Mamoré, Ji-Paraná, Dos Marmelos, Manicoré, Mataurá, Mariepauá, Aripuanã
Tawimito upande wa kushoto Mto Madre de Dios
Mkondo wastani m3/s 31,200, ⁃ wa chini m3/s 2,346, wa juu m3/s 52,804
Eneo la beseni km2 850,000
Mto Madeira

Mto Madeira (kwa Kireno: Rio Madeira; kabla ya ukoloni uliitwa na wenyeji kwa jina asilia Cuyari: [1] ) ni mto mkubwa katika Amerika Kusini. Una urefu wa km 3,250.[2] Madeira ni sehemu ya mfumo wa Mto Amazonas ukichangia asilimia 15 ya maji yote ya mto huO.[3]

Tabianchi ya beseni lake

[hariri | hariri chanzo]
Beseni la Mto Madeira.

Usimbishaji katika beseni la Madeira unacheza baina ya cm/m2 75 na cm/m2 300. Karibu na chanzo chake, Madeira ni mmoja kati ya mito mikubwa duniani ukibeba mkondo wa maji wa m3/s 18,000, takriban nusu ya kiasi cha Mto Kongo. Robo ya maji hayo inatiririka kwenye mitelemko ya milima ya Andes ya Bolivia. [4]

Njia ya usafiri

[hariri | hariri chanzo]

Maji ndani ya mto Madeira hucheza sana; wakati wa mvua usawa wake unapanda juu mita 15, na meli kutoka baharini zinaweza kuingia hadi Porto Velho, Brazil, ambayo ni umbali wa kilomita 1800 kutoka Bahari Atlantiki. Lakini katika miezi ya ukame maji hupungua na mto unapitika kwa vyombo vidogo tu visivyoingia chini ya maji zaidi ya mita 2.

Leo hii ni kati ya njia za maji zinazotumiwa zaidi ndani ya nchi ya Brazil na takriban tani milioni 4 za nafaka zinapelekwa nje ya nchi kupitia Mto Madeira.

  1. "Peru, Amazones. - David Rumsey Historical Map Collection". www.davidrumsey.com. Iliwekwa mnamo 16 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Madeira (river)". Talktalk.co.uk Archived 16 Januari 2014 at the Wayback Machine. (encyclopedia). Accessed May 2011.
  3. "Waters". Amazon Waters. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-29. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Seyler, Patrick. "Hydrological Control on the Temporal Variability of Trace Element Concentration in the Amazon River and its Main Tributaries". Geological Survey of Brazil (CPRM). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-21. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Madeira kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.