N'Djamena
Jiji la N'Djamena | |
Nchi | Chad |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,093,492 |
Ndjamena ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa nchini Chad ikiwa na wakazi 1,093,492 mnamo mwaka 2013.[1]
Ndani ya manisipaa kuna hara au mitaa kumi.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Zamani mji ulijulikana kwa jina la "Fort Lamy". Tangu mwaka 1973 jina limekuwa Ndjamena, N'Djaména, N'Djamena au Ndjaména.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Mji wa Ndjamena uko mahali ambako mito ya Chari na Logone inaungana. Ng'ambo ya mto uko mji wa Kousseri nchini Kamerun.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ndjamena ilianzishwa na Mfaransa Émile Gentil tarehe 29 Mei 1900 kama kambi ya kijeshi ikiitwa Fort-Lamy kama kumbukumbu ya kamanda Amédée-François Lamy aliyeuawa vitani kwenye mapigano ya Kousseri siku chache kabla ya kuanzishwa kwa Fort Lamy[2][3] .
Jina lilibadilishwa na rais François Tombalbaye kuwa Ndjamena mwaka 1973. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Chad 1979 / 1980 mji uliharibika na wakazi wengi waliondoka mjini lakini katika miaka ya baadaye wengine wengi waliingia.[4]
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Mji ulikua sana na haraka. Huduma za maji, umeme na makao havitoshi tena.
Mwaka * Idadi ya Wakazi
Makabila na vikundi mjini mwaka 1993:
- Waarabu wa Chad : 11,08 %
- Ngambay : 16,41 %
- Hadjeray : 9,15 %
- Daza : 6,97 %
- Bilala : 5,83 %
- Kanembou : 5,80 %
- Maba : 4,84 %
- Kanouri : 4,39 %
- Gor : 3,32 %
- Kouka : 3,20 %
- Sar : 2,24 %
- Barma : 2,10 %
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Ndjamena ni kitovu cha uchumi wa Chad.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Ndjamena ina vyuo na shule mbalimbali kama vile.
Shule za Sekondari (Lycée) :
- Lycée Félix Éboué (ya serikali)
- Lycée technique commercial (ya seriali)
- Lycée du Sacré-Cœur (binafsi - kikatoliki)
- Lycée-Collège évangélique (binafsi kiprotestant)
- Lycée Ibnou - Cinna (Kifaransa - Kiarabu)
- Lycée Roi Faycal (Kiarabu)
- Lycée Koweitien (Kiarabu)
- Lycée d'Amérigue (ya serikali)
- Lycée de Farcha (ya serikali)
- Lycée Technique Industrielle
- Lycée du Pont de Chagoua
- Lycée de Waliya
- Lycée de La Liberté
- Lycée de la Gendarmerie, etc.
Vyuo Vikuu (Université) :
- Université de Ndjamena (ya serikali)
- créée en 1970
- Université Roi Fayçal (binafsi - kiislamu)
Taasisi za elimu ya juu (École Supérieure) :
- ISSED - Institut Supérieur des Sciences de l'Éducation
- ENAM - École Nationale d'Administration et de Magistrature
- EIE - École Supérieure d'Électronique et d'Informatique
- ENASS - École Nationale des Sciences Infirmières et Sociales
- INJS - Institut Supérieur de la Jeunesse et des Sports
- ENS - École Normale Supérieure
- ENTP - École Nationale des Travaux Publics
- ISTAP - Institut Supérieur des Techniques Appliquées
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Cahiers de l'Afrique de l'Ouest Dynamiques de l'Urbanisation Africaine 2020: Africapolis, Une Nouvelle Géographie Urbaine. OECD. 20 fevereiro 2020
- ↑ Roman Adrian Cybriwsky, Capital Cities around the World: An Encyclopedia of Geography, History, and Culture, ABC-CLIO, USA, 2013, p. 208
- ↑ Zurocha-Walske, Christine (2009). Chad in Pictures. Twenty-First Century Books. uk. 17. ISBN 978-1-57505-956-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-30. Iliwekwa mnamo 2015-11-15.
- ↑ Samuel Decalo, Historical Dictionary of Chad, Scarecrow, 1987, pp. 229–230