Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Niger (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Niger
Mto Niger huko Kulikoro (Mali)
Mto Niger huko Kulikoro (Mali)
Chanzo Futa Djalon, Guinea
Mdomo Atlantiki
Nchi za beseni ya mto Guinea, Mali, Niger, Benin na Nigeria
Urefu 4,374 km
Kimo cha chanzo 800 m
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 6,000 m³/s
Eneo la beseni (km²) 1,900,000 km²

Niger ni mto mkubwa kabisa wa Afrika ya Magharibi na mto mrefu wa tatu barani Afrika ukiwa na mwendo wa km 4.374. Njia yake ni kama upinde ikianza Guinea katika nyanda za juu za Futa Djallon kuelekea kaskazini-mashariki kupitia Mali hadi Niger. Karibu na mji wa Timbuktu inageukia kuelekea mashariki, halafu mashariki-kusini kupitia Benin na Nigeria hadi kufika mdomo wa delta yake kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki.

Kabla ya kufikia Timbuktu (Niger) mto unapanuka kuwa na delta ya barani pia mdomo wake baharini una delta kubwa sana.

Jina linatokana na lugha ya Watuareg "ghir n-igheren" (yaani "Mto wa mito")[1]. Jina hili lilichukuliwa na waandishi wa Ulaya ya karne za kati na kusomwa kwa namna ya Kilatini kama "Niger" yaani "cheusi", "mto mweusi" au "mto wa nchi ya Weusi". Jina hili la Kilatini lilionekana mara ya kwanza kwenye ramani ya Klaudio Ptolemaio kwa ajili ya mto mmoja upande wa kusini wa milima ya Atlas.

Nchi za kisasa za Niger na Nigeria zimepata majina yake kutoka kwa jina la mto huo. Wenyeji wa huko wana majina mbalimbali kwa ajili ya mto huu: Joliba katika lugha za Kimandinga na Isa Ber kwa Kisonghai. Majina yote humaanisha "mto mkubwa". Katika maeneo karibu na mdomo wake ulijulikana pia kama "Kworra" (au Quorra).

Wataalamu wa Ulaya waliokusanya habari zake walifikiri mwanzoni ya kwamba unaishia kwenye Ziwa Chad au katika mto Naili. Walitambua baadaye ya kwamba ni mto uleule uliojulikana kwao tayari kwa jina la "Quorra".

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Njia ya upinde ya mto Niger ilichanganya wataalamu wa Ulaya pamoja na Waarabu kwa karne nyingi. Waroma wa kale walifahamu mto ule mkubwa karibu na Timbuktu wakafikiri ya kwamba unaendelea kujiunga na mto Nile. Mtaalamu Mwarabu Ibn Battuta alifikiri hivyo pia.

Wengine waliona utaishia kwenye mto Senegal au mto Kongo. Kuchanganyikiwa huku kulisababisha kwa karne nyingi ramani zisizoonyesha mwendo halisi wa mto. Wasafiri na wataalamu wa nje hawakuelewa ya kwamba mto mkubwa ulio karibu na Timbuktu na mto mkubwa unaoingia Atlantiki kwenye Ghuba ya Guinea huko Nigeria ni mto uleule.

Ni tangu mwaka 1830 tu ya kwamba msafara wa mpelelezi Mungo Park ulileta taarifa ya kutambua hali halisi.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Mto Niger una chanzo chake katika milima ya Futa Djalon nchini Guinea, umbali wa kilomita 240 kutoka bahari Atlantiki. Lakini haufiki baharini moja kwa moja, bali unaelekea kaskazini mashariki kwa Sahara kupitia Bamako na kuunda delta ya barani inayoitwa "Massina" ambako mji mkubwa ni Mopti. Unaendelea hadi Timbuktu unapopita kwenye Sahara ya kusini na kubadilisha mweleko kwenda kusini mashariki. Karibu na mji wa Gao unapita kwa matuta ya mchanga ya Koyma na kuingia tena katika kanda la Sahel. Halafu unapita nchi ya Niger na mji mkuu wake, Niamey. Kutoka hapa njia yake ni mpaka wa Benin hadi "hifadhi ya W" mpakani mwa Niger, Burkina Faso na Benin. Kutoka hapa mto Niger unaendelea hadi Nigeria. Karibu na Lokoja unapokea tawimto wa Benue na kuingia katika kanda la msitu wa mvua wa Nigeria. Karibu na mji wa Onitsha mto unaanza kujigawa na kuwa delta ya Niger. Mikono yake mikubwa inaitwa Forcados, Nun na Escravos.

Upinde mkubwa wa mto Niger unavyoonekana kutoka satelaiti ni upinde wa kijani katika nchi kavu yenye rangi ya kahawia ya Sahel na Sahara.

Mto Niger unabeba matope kidogo kulingana na mto Naili kwa sababu chanzo chake kipo katika eneo la miamba.[2]}} Sawa na Naili ina mafuriko ya kila mwaka yanayoanza mwezi wa Septemba, kufikia jii kwenye Novemba na kuishi mwezi wa Mei [3]

Tabia isiyo ya kawaida ni delta ya barani inayotokea pale ambako mtelemko wa mto unakwisha. Tokeo lake ni eneo lenye ukubwa wa Ubelgji ambako mto unagawiwa katika mikono mingi na vinamasi. Hili ni eneo zuri kwa uvuvi na kilimo. [4]}}

Kati ya delta ya barani na Timbuktu mto unapotewa na angalau theluthi mbili za maji yake katika ardhi kavu pamoja na uvukizaji. Upotevu huu umekadiriwa kulingana na km3 31 kwa mwaka lakini kiasi kinabadilika mwaka kwa mwaka. [5]

Baadaye matawimto mengi yanaingia na kuongeza kiwango cha maji, hata hivyo kiasi kikubwa kinapotea kwa sababu ya uvukizaji.

Hidrolojia

[hariri | hariri chanzo]

Kiwango cha maji kwenye mto kinategemea majira: kuna tofauti kubwa kati ya majira ya mvua na ukame. Kiasi kilipimwa kwa muda wa miaka 40 kwenye mji wa Malanville nchini Benin uliopo kilomita 1100 kutoka mdomo wa mto. [6] Katika kipindi hicho wastani wa maji katika miaka hii 49 ilikuwa m³/s 1053; kiasi kidogo kilikuwa m³/s 18, inayomaanisha mto karibu kukauka. Kiasi cha juu kilikuwa m³/s 2726. Kwa wastani ni m³/s 6000 zinazofikia Atlantiki.

Feri ya mto Niger karibu na mji wa Mopti

Matawimto

[hariri | hariri chanzo]
Beseni la mto Niger.

Miji mtoni

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Hunwick, John O. (2003) [1999]. Timbuktu and the Songhay Empire: Al-Sadi's Tarikh al-Sudan down to 1613 and other contemporary documents. Leiden: Brill. p. 275 Fn 22. ISBN 90-04-11207-3.
  2. Reader, John (2001), Africa, Washington, D.C.: National Geographic Society, ISBN 0-620-25506-4. uk.191
  3. Reader uk. 191
  4. Reader uk. 191–192
  5. FAO:Irrigation potential in Africa: A basin approach, The Niger Basin, 1997
  6. GRDC – Mto Niger huko Malanville
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Niger (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.