Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Nomino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • Anna na Juma wanacheza.
  • Gari la Oliver' ni zuri sana.
  • Nyumba yetu ipo mjini.
  • Mbuzi wa jirani yetu.
  • Mti mrefu umekatika.

Nomino (kutoka Kilatini: nōmen, jina) ni aina ya maneno inayotaja jina la mtu, mnyama, kitu, mahali, sifa au wazo. Nomino hutokea kwa umbo la umoja au uwingi: kitu, vitu; mtu, watu.

Nomino pamoja na kitenzi hufanya sentensi, mfano: mtu anatembea.

Makundi ya nomino

Nomino zimeainishwa katika makundi mbalimbali - kutegemeana na mitazamo ya wataalamu. Pamoja na kuwepo kwa msigano baina yao, bado wataalamu wengine wameziainisha nomino (majina) katika makundi matano:

  1. Nomino za pekee
  2. Nomino za kawaida - (vilevile jamii)
  3. Nomino za dhahania - (vilevile maarifa)
  4. Nomino za jumla
  5. Nomino za wingi

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nomino kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.