Pamba
Pamba ni nyuzi nyeupe na laini zinazotokana na tunda la mpamba (Gossypium sp.). Nyuzi hizi zinaonekana kama sufi na mipamba inalimwa kwa nyuzi hizi ambazo ni msingi wa kutengeneza kitambaa na nguo.
Ndani ya tunda nyuzi za pamba zinaunganishwa na punje za mbegu wa mmea. Kusudi yao ni kusambaza mbegu kwa sababu zinafanya kazi kama tanga zinashika nguvu ya upepo na kuwezesha mbegu kuelea hewani mbali kiasi.
Pamba yenyewe inapatikana kutoka spihi nyingi za gossypium zinazokua kiasili katika sehemu mbalimbali za dunia. Lakini karibu pamba yote inayolimwa kwa matumizi ya nguo imetokana na spishi nne za mipamba ambazo ni
- Gossypium herbaceum L. (asili ya Asia)
- Gossypium arboreum L. (asili ya Asia)
- Gossypium hirsutum L. (asili ya Amerika)
- Gossypium barbadense L. (asili ya Amerika).
Kitambaa cha pamba huwa na faida nyingi kuliko vitambaa vya sintetiki. Pamba inaweza kushika unyevu hadi asilimia 80% ya uzito wake hivyo kitambaa chake kinapendeza hasa katika mazingira ya joto kwa sababu mtu husumbuliwi sana na jasho.
Mavuno duniani 2004/2005
[hariri | hariri chanzo]2004/2005 jumla ya tani 26.043.000 t za pamba zilivunwa duniani. Nchi zenye mavuno kubwa zilikuwa zifuatazo:
Nchi zenye mavuno makubwa ya pamba (2004/05) | |||
Rang | Nchi | Mavuno (kwa t elfu) | Asilimia ya mavuno ya dunia |
---|---|---|---|
1 | China | 6.320 | 24,27 % |
2 | USA | 5.062 | 19,44 % |
3 | Uhindi | 4.080 | 15,67 % |
4 | Pakistan | 2.415 | 9,27 % |
5 | Brasilia | 1.250 | 4,80 % |
6 | Usbekistan | 1.134 | 4,36 % |
7 | Afrika ya Magharibi1 | 1.040 | 3,99 % |
8 | Uturuki | 900 | 3,46 % |
9 | Australia | 613 | 2,35 % |
10 | Ugiriki | 390 | 1,50 % |
11 | Syria | 331 | 1,27 % |
12 | Misri | 291 | 1,12 % |
13 | Turkmenistan | 203 | 0,78 % |
14 | Tajikistan | 172 | 0,66 % |
15 | Kazakhstan | 148 | 0,57 % |
Wengine | 1.694 | 6,51 % | |
Dunia yote | 26.043 | 100,00 % | |
(1) Afrika ya Magharibi inajumlisha Benin (152), Burkina Faso (257), Kamerun (105), Chad (85), Cote d'Ivoire (130), Mali (240) na Togo (71) |
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pamba kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |