Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Plastiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vifaa vya nyumbani vilivyotengenezwa kwa plastiki

Plastiki (kutoka Kigiriki πλαστική plastiki yaani "iliyopewa umbo fulani" ) ni aina ya maunzi mango yanayoundwa kwa njia ya kikemia na kukubali umbo lolote yakiwa teke.

Plastiki ni maunzi sintetiki ambayo haitokei katika mazingira kiasili. Inatengenezwa kwa kuunganisha molekuli nyingi kuwa nyororo ndefu ya polima.

Kuna aina nyingi za plastiki. Kwa kuchagua kemikali na kuongeza madawa mbalimbali kuna chaguo kubwa ya tabia kama ugumu, kubadilika umbo, unyumbufu, uvumilivu kwa joto au baridi au muda wa kudumu.

Wakati wa kutengenezwa plastiki inakubali kila umbo hivyo hutolewa kama filamu, punje, vipande bapa au umbo lolote linalotakiwa. Mifuko na maunzi ya kufugia bidhaa huwa ni plastiki. Plastiki haipokei maji au unyevu hivyo kitu kinachofungwa kabisa ndani ya karatasi ya plastiki inabaki kavu.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Maunzi ya kwanza katika historia yaliyofanana na plastiki ilikuwa aina ya lami iliyopatikana baada ya kupika utomvu ya miti fulani. Baadaye wataalamu walibuni njia za kubadilisha vitu kama pembe ya wanyama kwa kuipika pamoja na madawa ilikukubali kubadilishwa umbo.

Hatua kubwa ilikuwa mbinu wa kutia dawa la sulfuri kwenye mpira asilia. Kwa njia hii Charles Goodyear wa Marekani aliweza kutengeneza mpira ulioendelea kuwa laini. Aliendelea kubuni njia ya kubadilisha tabia za mpira kuwa mgumu kabisa.

Maendeleo makubwa ya plastiki ilipatikana na utaalamu wa kutumia mafuta ya petroli. Mafuta haya mazito ni mchanganyiko wa kemikali mbalimbali. Katika viwanda vya kusafishia mafuta maunzi haya yanatenganishwa na molekuli zinazofaa zinatolewa kwa matenegnezo ya aina za plastiki.

Aina za Plastiki

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya wastani ya plastiki kwa kila mkazi yalikuwa mwaka 2000:

Hadi mwaka 2017 mnamo tani bilioni 8.3 zilitengenezwa duniani. Tani milioni 6.3 za jumla hii zimekuwa takataka isiyotumiwa tena. Asilimia 9 ya takataka hiyo zilirejereshwa na kutumiwa tena kwa umbo tofauti. Asilimia 12 zilichomwa na asilimia 79 ziliwekwa kwenye dampo za takataka au kukaa katika mazingira.

Matatizo ya mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Plastiki huoza polepole sana. Hii inasababisha machafuko ya mazingira hasa pasipo na huduma za takataka. Aina nyingi zikichomwa zinatoa gesi za sumu. Matengenezaji wa Plastiki yanahitaji matumizi ya kemikali nyingi za sumu ambazo ni hatari kwa mazingira.

Hivyo nchi nyingi zimeanza kutoa sheria juu ya matumizi ya plastiki.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Plastiki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.