Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Polima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Molekuli ya selulosi ni polima
Vitu vilivyotengenezwa polyethilini ya polima na polypropylene.

Polima (kutoka Kiingereza "polymer") ni molekuli ndefu iliyotengenezwa kwa kuungana pamoja vizio vingi vidogo vya kemikali.

Jina polima linatokana na neno ambalo ni la Kigiriki cha kisayansi lililopatikana kwa kuunganisha πολύ poli ‘nyingi‘ na μέρος meros ‘sehemu, kizio‘ kwa hiyo kumaanisha "ya vizio vingi". Hii inaonyesha jinsi muundo wa polima unavyokuwa na vizio vingi vidogo vilivyounganishwa pamoja kuwa molekuli kubwa.

Mmenyuko wa kikemia unaounganisha vizio vya kemikali kuunda polima huitwa upolimishaji.

Polima asilia

[hariri | hariri chanzo]

Polima nyingine ni za asili na zinafanywa na viumbe. Protini zina molekuli za polipeptidi. Hizi ni polima asilia zinazounganisha vizio vya asidi amino.

Selulosi na wanga (zote mbili ni kabohidrati) pia ni polima asilia zinazounganisha vizio vya glukosi. Mpira ni mchanganyiko wa polima asilia.

Polima zinazotegnezewa

[hariri | hariri chanzo]

Plastiki ni polima zilizotengenezwa na mwanadamu. Nyuzi nyingi zinafanywa na polima.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Polima kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.