Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Selulosi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Selulosi.

Selulosi (kutoka neno la Kiingereza "cellulose") ni tishu iundayo sehemu kubwa ya miti na mimea mingine.

Kikemia inaundwa na sehemu nyingi za glukosi yenye fomula (C6H10O5)n zinazounganishwa kuwa molekuli ndefu (polima).

Selulosi inapatikana zaidi kwenye mimea ya rangi ya kijani na inatengeneza kiwambaseli cha mmea.

Selulosi haiwezi kuliwa na wanyama lakini spishi kadhaa, kama vile mchwa na ng'ombe, hutunza bakteria katika matumbo yao wanaovunja molekuli za selulosi kwa sehemu ndogo zaidi zinazoweza kumeng’enywa.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Selulosi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.