Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Rula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya kifaa kiitwacho rula.

Rula (kutoka Kiingereza "ruler") ni kifaa kinachotumika kupima urefu. Kizio cha kawaida cha kupima urefu ni Mita (m).

Hata hivyo, mita si kizio pekee cha kupima urefu, kuna vizio vingine kama vile Kilometa, sentimeta, Milimita na vilevile Maili n.k. ambayo hutumika kupika urefu.

Rula hutengenezwa kwa aina mbalimbali na urefu tofauti. Baadhi ni za mbao, chuma au plastiki. Rula fupi ni bora kwa kuweka mfukoni, wakati nyingine ni ndefu kwa matumizi mbalimbali.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Rula ya mbao ya seremala na zana nyingine zilizopatikana karne ya 16.

Rula zilianza kutumika miaka mingi iliyopita. Ufito wa shaba wa kupimia wa kale kabisa ni wa mwaka 2650 KK na ulivumbuliwa na Mjerumani Eckhard Unger huko Nippur.

Rula zilizotengenezwa kwa pembe ya ndovu zilitumiwa kwenye Ustaarabu wa Bonde la Indus kabla ya 1500 KK. Rula ya aina hii ilipatikana wakati wa uchimbaji huko Lothal (2400 KK) ikiwa na milimita 1.6.

Anton Ullrich alivumbua rula ya kukunja mwaka 1851. Frank Hunt alivumbua rula inayopindika mwaka 1902.[1]

Faida za rula

[hariri | hariri chanzo]

1) hutumika kupima urefu wa kitu

2) hutumika katika kuchora

  1. "Flexible Ruler Invented by Frank G. Hunt". National Museum of National History. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rula kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.