Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Upumuo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Video ya mnyama wa kike jamii ya mamba akipumua.

Upumuo ni kitendo cha kuvuta hewa ndani ya mapafu au oksijeni kupitia viungo vingine kama vile matamvua ya samaki, halafu kutoa gesi ya CO2 pamoja na hewa iliyotumiwa.

Kuna pia upumuo wa ndani ambayo ni kazi ya seli za mwili kupokea oksijeni na kuitumia kwa mchakato wa oksidisho ndani yao.

Kazi ya mapafu katika upumuo
(Njia ya hewa inaanza mdomoni na puani ; musuli za kiwambo tumboni (njano-nyekundu) zinajikaza au kulegeza na hivyo kupanua au kupunguza ukubwa wa mapafu (bluluu nyeupe/zambarau)

Hewa ya kuvutwa ndani na ya kutoka nje

[hariri | hariri chanzo]

Binadamu hupumua takriban mara 23,000 kila siku akihamisha mita za mjazo 12.5 kwa jumla.

  • Hewa tunayovuta ndani ya mapafu ni hewa ya kawaida yenye asilimia 78 % za nitrojeni, 21 % za oksijeni, mvuke wa maji, gesi adimu kwa viwango vidogo na 0,04 % dioksidi kabonia (CO2).
  • Hewa tunayotoa nje bado ina asilimia 78 % za nitrojeni, lakini ni 16 % za oksijeni pekee zilizobaki na dioksidi kabonia imekuwa 4 %.
  • Asilimia kubwa ya oksijeni iliyopungua imeoksidisha na glukosi ndani ya seli za mwili kwa kutengeneza nishati.

Njia za upumuo

[hariri | hariri chanzo]

Jumla ya sehemu za mwili zinazohusika na upumuo huitwa mfumo wa upumuaji.

Kwa wanyama wenye mapafu hewa inavutwa ndani kupitia mdomo au pua. Hewa hii huitwa pumzi.

Kazi hii inatekelezwa kwa njia ya kukaza au kulegea kwa musuli za kiwambo cha tumboni kinachotenganisha tumbo na nafasi ya mapafu. Mabadiliko haya yanabadilisha nafasi ya mapafu na shindikzo ndano yao na kusababisha kuvutwa au kusukumwa kwa hewa.

Kwa samaki na wanyama wengine wanaoishi chini ya maji wenye matamvua maji yenye hewa ndani yake inapitishwa kwenye majani ya ngozi zinazofanya matamwua na hewa inapokelewa na vyombo vya damu kupitia ngozi ya matamvua ambayo ni nyembamba sana. Kuna pia wadudu kadhaa kwenye nchi kavu wenye matamvua.

Wadudu huwa na mabomba membamba (ing. trachea) yanayoelekea ndani ya miili yao na hewa inaingia hapa; ngozi nyembamba ndani ya mwili inaruhusu kuingia kwa oksijeni mwilini.

Wanyama wadogo sana wanatosheleka kupokea oksijeni kupitia ngozi pekee kwa hiyo hawana mapafu wala trachea. Wote wanaotumia njia hii wana umbo bapa sana au umbo la minyoo pia wanaishi katika mazingira penye unyevu. Mfano ni nyungunyungu.

  • Parkes M (2006). "Breath-holding and its breakpoint". Exp Physiol. 91 (1): 1–15. doi:10.1113/expphysiol.2005.031625. PMID 16272264. Full text
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upumuo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.