Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Waturuki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waturuki: Mehmed II- Suleiman Mkuu - Mustafa Kemal Atatürk - Sabiha Gökçen - Wakinadada Pekinel
Cahit Arf - Nazım Hikmet - İdil Biret - Oktay Sinanoğlu - Şebnem Ferah

Waturuki ni jina la raia wote wa nchi ya Uturuki. Wakazi wa Uturuki ni milioni 78 hivi, lakini si wote Waturuki kiutamaduni: wengine (20-30%) ni Wakurdi, halafu wako Waarabu, Waarmenia n.k.

Waliohamia nchi nje ya Uturuki pamoja na watoto wao ni takriban milioni 7: wengi wao wako Ujerumani.

Waturuki walio wengi ni Waislamu Wasunni, lakini kuna tofauti kati yao. Wengine (labda 25%) ni Waalevi ambao ni tawi la Washia. Wakristo waliokuwa kundi kubwa kihistoria wamebaki wachache baada ya Maangamizi ya Waarmenia na kuwafukuza na kuwahamisha Wagiriki baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Wanaongea lugha ya Kituruki ambayo ni lugha kubwa katika familia ya lugha za Kiturki (Turkic languages). Kati ya mataifa ya Waturki (Turkic peoples) Waturuki (Turks) ni kundi kubwa kabisa.

Katika utafiti wa urithi wa kinasaba (DNA) imeonekana kuwa Waturki hawana asili moja, maana wasemaji wa lugha za Kiturki walioingia maeneo hayo miaka 1.000 iliyopita hawakuwa wengi sana, wakatawala wakazi asilia waliosema Kigiriki, Kiarmenia na lugha nyingine nyingi hata polepole wengi walianza kutumia lugha ya Kituruki. Kwa hiyo asili zao ni tofauti sana, ila wameunganishwa na lugha, utamaduni na dini.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waturuki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.