Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Faksi Quotes

Quotes tagged as "faksi" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Kamishna … karibu," alisema Nafi huku akisimama na kutupa gazeti mezani na kuchukua karatasi ya faksi, iliyotumwa.
"Ahsante. Kuna nini …"
"Kamishna, imekuja faksi kutoka Oslo kama nilivyokueleza – katika simu. Inakutaka haraka, kesho, lazima kesho, kuwahi kikao Alhamisi mjini Copenhagen," alisema Nafi huku akimpa kamishna karatasi ya faksi.
"Mjini Copenhagen!" alisema kamishna kwa kutoamini.
"Ndiyo, kamishna … Sidhani kama kuna jambo la hatari lakini."
"Nafi, nini kimetokea!"
"Kamishna … sijui. Kwa kweli sijui. Ilipofika, hii faksi, kitu cha kwanza niliongea na watu wa WIS kupata uthibitisho wao. Nao hawajui. Huenda ni mauaji ya jana ya Meksiko. Hii ni siri kubwa ya tume kamishna, na ndiyo maana Oslo wakaingilia kati."
"Ndiyo. Kila mtu ameyasikia mauaji ya Meksiko. Ni mabaya. Kinachonishangaza ni kwamba, jana niliongea na makamu … kuhusu mabadiliko ya katiba ya WODEA. Hakunambia chochote kuhusu mkutano wa kesho!"
"Kamishna, nakusihi kuwa makini. Dalili zinaonyesha hali si nzuri hata kidogo. Hawa ni wadhalimu tu … wa madawa ya kulevya."
"Vyema!" alijibu kamishna kwa jeuri na hasira. Halafu akaendelea, "Kuna cha ziada?"
"Ijumaa, kama tulivyoongea wiki iliyopita, nasafiri kwenda Afrika Kusini."
"Kikao kinafanyika Alhamisi, Nafi, huwezi kusafiri Ijumaa …"
"Binti yangu atafukuzwa shule, kam …"
"Nafi, ongea na chuo … wambie umepata dharura utaondoka Jumatatu; utawaona Jumanne … Fuata maadili ya kazi tafadhali. Safari yako si muhimu hivyo kulinganisha na tume!"
"Sawa! Profesa. Niwie radhi, nimekuelewa, samahani sana. Samahani sana.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“John Murphy amefariki dunia. Ndege aliyotoka nayo hapa, Dar es Salaam, ndiyo aliyotoka nayo Paris na ndiyo hiyo iliyoanguka katika mazingira ya kutatanisha. Watu waliobahatika kuing’amua fununu hii ni wachache na ambao hivi sasa hawajiwezi kabisa, akiwemo kamishna wetu wa kanda Profesa Mafuru. Profesa yuko mahututi. Ameshtuka baada ya kusikia taarifa hizo katika redio ya hapa. Yuko chini ya uangalizi mkali wa madaktari. Mungu aiweke roho ya John Murphy, shujaa wa karne, mahali pema peponi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita