Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Simu Quotes

Quotes tagged as "simu" Showing 1-7 of 7
Enock Maregesi
“Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Israeli Daniel Yehuda Ben-Asher Ebenezer, Mhebrania aliyeishi Givat Ram, Jerusalem, na mke wake mrembo Hadara na mtoto wake mzuri Navah Ebenezer, alikuwa Ukanda wa Gaza siku alipopigiwa simu na Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia U Nanda – kutoka Copenhagen kuhusiana na wito wa haraka wa kuonana na Rais wa Tume ya Dunia. Yehuda aliondoka usiku kwenda Yangon, Myama, ambapo alionana na U Nanda na kupewa maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata. Mbali na maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata, Nanda alimkabidhi Yehuda kachero wa Kolonia Santita Mandi Dickson Santana (bila kujua kama Mandi ni kachero wa Kolonia Santita) ili amsindikize mpaka stendi ya mabasi ya Maubin, nje ya Yangon. Baada ya hapo Yehuda alisafiri mpaka Copenhagen ambapo yeye na wenzake walikabidhiwa Operation Devil Cross, ya kung’oa mizizi ya Kolonia Santita duniani kote. Yehuda alifanya kosa kubwa kuonana na kachero wa Kolonia Santita Mandi Santana! Kwa sababu hiyo, sauti na picha ya Yehuda vilichukuliwa, watu wengi walikufa katika miji ya Copenhagen na Mexico City.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini kabla Rais hajaendelea kuongea, na ‘John Murphy wa Kolonia Santita’, Mogens aliruka na kumnyang’anya simu.
“Ambilikile,” Mogens aliita, akiangalia saa.
“Brodersen,” Sauti ya upande wa pili ilijibu, baada ya sekunde kumi.
“60111906,” Mogens alisema, baada ya sekunde kumi.
“57121906,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi.
“Jumapili,” Mogens aliendelea, baada ya sekunde kumi.
“Ijumaa,” Sauti ya upande wa pili ikajibu, baada ya sekunde kumi.
John Murphy wa Kolonia Santita aliposema ‘Ijumaa’, Mogens aliunda kicheko na kurusha mkono katika matundu ya kuongelea ya simu ...”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Mapema, kabla ndege haijaondoka na baada ya kuagana na maafisa waliomsindikiza, Nanda aliingia katika ndege na kutafuta namba ya kiti chake. Alivyoiona, alishtuka. Msichana mrembo alikaa kando ya kiti (cha Nanda) akiongea na simu, mara ya mwisho kabla ya kuondoka. Alivyofika, Nanda hakujizuia kuchangamka – alitupa tabasamu. Alivyoliona, kupitia miwani myeusi, binti alitabasamu pia, meno yake yakimchanganya kamishna. Alimsalimia Nanda, harakaharaka, na kurudi katika simu huku Nanda akikaa (vizuri) na kumsubiri. Alivyokata simu, alitoa miwani na kumwomba radhi Kamishna Nanda. Nanda akamwambia asijali, huku akitabasamu. Alikuwa na safari ya Bama kupitia Tailandi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Skandinavia na Maxair kutokea Bangkok; sawa kabisa na safari ya kamishna.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Kamishna … karibu," alisema Nafi huku akisimama na kutupa gazeti mezani na kuchukua karatasi ya faksi, iliyotumwa.
"Ahsante. Kuna nini …"
"Kamishna, imekuja faksi kutoka Oslo kama nilivyokueleza – katika simu. Inakutaka haraka, kesho, lazima kesho, kuwahi kikao Alhamisi mjini Copenhagen," alisema Nafi huku akimpa kamishna karatasi ya faksi.
"Mjini Copenhagen!" alisema kamishna kwa kutoamini.
"Ndiyo, kamishna … Sidhani kama kuna jambo la hatari lakini."
"Nafi, nini kimetokea!"
"Kamishna … sijui. Kwa kweli sijui. Ilipofika, hii faksi, kitu cha kwanza niliongea na watu wa WIS kupata uthibitisho wao. Nao hawajui. Huenda ni mauaji ya jana ya Meksiko. Hii ni siri kubwa ya tume kamishna, na ndiyo maana Oslo wakaingilia kati."
"Ndiyo. Kila mtu ameyasikia mauaji ya Meksiko. Ni mabaya. Kinachonishangaza ni kwamba, jana niliongea na makamu … kuhusu mabadiliko ya katiba ya WODEA. Hakunambia chochote kuhusu mkutano wa kesho!"
"Kamishna, nakusihi kuwa makini. Dalili zinaonyesha hali si nzuri hata kidogo. Hawa ni wadhalimu tu … wa madawa ya kulevya."
"Vyema!" alijibu kamishna kwa jeuri na hasira. Halafu akaendelea, "Kuna cha ziada?"
"Ijumaa, kama tulivyoongea wiki iliyopita, nasafiri kwenda Afrika Kusini."
"Kikao kinafanyika Alhamisi, Nafi, huwezi kusafiri Ijumaa …"
"Binti yangu atafukuzwa shule, kam …"
"Nafi, ongea na chuo … wambie umepata dharura utaondoka Jumatatu; utawaona Jumanne … Fuata maadili ya kazi tafadhali. Safari yako si muhimu hivyo kulinganisha na tume!"
"Sawa! Profesa. Niwie radhi, nimekuelewa, samahani sana. Samahani sana.”
Enock Maregesi, Kolonia Santita

Enock Maregesi
“Hata kama unadaiwa, pokea simu ukipigiwa. Unaweza kupoteza fursa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nisipopiga simu hupigi. Usipopiga sipigi. Hicho ni kiburi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama kuna jambo la muhimu unapaswa kufanya kwa ajili ya kadari ya maisha yako na kipindi hichohicho kuna kipindi kizuri cha televisheni unakisubiria, au simu ya umbea, au kinanda cha shida, palilia bustani yako ya kiroho kwa kuachana na televisheni na simu na kufanya jambo la msingi kwa ajili ya maisha yako.”
Enock Maregesi