Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Albrecht Dürer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dürer alivyojichora mwenyewe mnamo 1498

Albrecht Dürer (21 Mei 1471 - 6 Aprili 1528) alikuwa mchoraji na mkata nakhshi] Mjerumani. Alifahamika pia kama mtaalamu wa hisabati, hasa jiometria. Ahesabiwa kama msanii muhimu zaidi wa zama ya mwamko katika Ulaya ya kaskazini.

Mitindo ya kazi

[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya kazi za Dürer ni chapisho za picha nakhshi katika ubao au shaba. Alichora pia picha kwa rangi za mafuta na rangi za maji.

Dürer alizaliwa mjini Nürnberg alipoishi na kufa. Wakati ule Nürnberg ilikuwa mji tajiri wa biashara ya kimataifa.

Baba yake alikuwa Mhungaria aliyemfundisha ufundi wa kuchonga dhahabu.

Alipokuwa kijana alifanya matembezi ya miaka mitano katika Ujerumani, Uholanzi na Uswisi alipoboresha sanaa yake.

Baadaye aliongeza safari ya kwenda Italia alipofanya kazi Venezia na kuona mengi.

Mwaka 1494 alifunga ndoa na Agnes Frey akafungua karakana yake. Kazi mashuhuri ya kwanza ilikuwa mfululizo wa picha nakhshi katika ubao 15 kuhusu Ufunuo wa Yohane.

Aliendelea kuchora picha nyingi za dini juu ya habari na watu wa Biblia. Lakini alitafutwa pia na matajiri na wakubwa waliotaka picha zao.

Kuanzia mwaka 1512 aliajiriwa mara nyingi na Kaisari Maximilian I.

Wikimedia Commons ina media kuhusu: