Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Tabora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 14:18, 17 Novemba 2023 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Mkoa wa Tabora
Mahali paMkoa wa Tabora
Mahali paMkoa wa Tabora
Mahali pa Mkoa wa Tabora katika Tanzania
Majiranukta: 5°30′S 32°50′E / 5.500°S 32.833°E / -5.500; 32.833
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Tabora
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa ACP Advera John Bulimba
Eneo
 - Jumla 76,151 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 3,391,679
Tovuti:  http://www.tabora.go.tz/

Ramani ya Mkoa wa Tabora na wilaya zake 7.

Tabora wakati wa ukoloni wa Wajerumani.

Mkoa wa Tabora ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 45000.

Makao makuu yako Tabora Mjini. Tabora ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania ya kati.

Eneo la mkoa ni km2 76,151; mnamo km2 34,698 (46%) ni hifadhi ya misitu, km2 17,122 (22%) ni hifadhi ya wanyama.

Jumla ya wakazi ilikuwa watu 3,391,679 (2022[1]). Wenyeji wa Tabora ni hasa Wanyamwezi. Walio wengi ni wakulima na wafugaji.

Kuna wilaya 8 (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022[2]): Tabora Mjini (308,741), Nzega Vijijini (574,498), Nzega Mjini (125,193), Igunga (546,204), Uyui (562,588), Urambo (260,322), Sikonge (335,686), Kaliua (678,447).

Jina la Urambo humkumbuka Mtemi Mirambo aliyekuwa mtawala muhimu wa Wanyamwezi kabla ya kuingia kwa ukoloni.

Barabara

[hariri | hariri chanzo]

Mkoa wa Tabora una barabara za lami. Ipo inayoanzia Tabora mjini hadi Nzega kuelekea Mwanza. Pia lami kutoka Nzega kuelekea Igunga mpaka Singida.

Barabara nyingine ya lami ipo inayoanzia Tabora mjini mpaka Urambo yenye urefu wa km 93.

Pia lami nyingine inaanzia Tabora mjini mpaka Manyoni yenye urefu wa km 254 ukipitia Itigi.

Kuna njia ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa upande moja na kwenda Mwanza kwa upande mwingine.

Majimbo ya bunge

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Tabora kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.