Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Yesu kutolewa hekaluni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 14:39, 26 Julai 2022 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango) (Katika liturujia)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Mkutano wa Bwana, Picha takatifu ya Urusi, karne ya 15.
Yesu kutolewa hekaluni, mchoro wa Giotto, Padova, Italia.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Yesu kutolewa hekaluni ni tukio la utoto wake, siku arubaini baada ya kuzaliwa, iliyopangwa na Torati kuwa siku ya kumtakasa mama yeyote aliyemzaa mtoto wa kiume.

Siku hiyo aliletwa na Yosefu na Maria katika hekalu la Yerusalemu ili atolewe kwa Mungu, akiwa mtoto wa kiume wa kwanza, akakombolewa kwa sadaka ya fukara. Ndipo alipotambuliwa na kutangazwa na wazee wawili watakatifu, Simeoni na Anna.

Katika Injili

[hariri | hariri chanzo]

Habari hiyo inasimuliwa na Luka mwinjili tu kama ifuatavyo:

Lk 2:22 Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Mose, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana. 23 Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: "Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana." 24 Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana.

25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. 26 Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Masiha wa Bwana. 27 Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia Hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na Sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu na kusema: 29 "Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani. 30 Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu utokao kwako, 31 ambao umeutayarisha mbele ya watu wote: 32 Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli."

33 Baba na mama yake Yesu walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto. 34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, "Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; 35 na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako."

36 Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa. 37 Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa Hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana. 38 Saa hiyohiyo alijitokeza mbele, akamshukuru Mungu, na akaeleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wanatazamia ukombozi wa Yerusalemu.

39 Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na Sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, mkoani Galilaya. 40 Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa pamoja naye.

Katika liturujia na Rozari

[hariri | hariri chanzo]

Tukio hilo linaadhimishwa na Wakristo wengi siku 40 baada ya Noeli.

Katika Ukristo wa magharibi sikukuu hiyo iliwahi kuitwa pia "Mweuo wa Bikira Maria"; siku yake ni tarehe 2 Februari[1].

Ukristo wa Mashariki unaiita “Mkutano”, kwa kuwa Yesu alikutana na hao wazee waliowakilisha watu wote wenye imani na furaha kwa kumuona yeye aliye mwanga wa mataifa na utukufu wa watu wake, Israeli.

Wanaosali Rozari wanalitumia tukio hilo kama fungu la nne kati ya mafumbo ya furaha kwa sababu linahusu utoto wa Yesu, ingawa habari yenyewe si ya kufurahisha bali zaidi ya kutia huzuni.

  • Schiller, Gertud, Iconography of Christian Art, Vol. I, 1971 (English trans from German), Lund Humphries, London, ISBN 0-85331-270-2
  • Food and Feast in Medieval England, P. W. Hammond, ISBN 0-7509-0992-7

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yesu kutolewa hekaluni kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.