Deuterokanoni
Vitabu vya deuterokanoni (kutoka Kigiriki "deuteros" = ya pili na "kanon" = orodha[1]) ni maandiko yanayotazamwa na Wakatoliki, na baadhi ya Waorthodoksi na ya Makanisa ya Kale ya Mashariki kama sehemu kamili ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo[2].
Vitabu hivyo viliandikwa miaka 300 - 50 KK[3][4][5].
Wayahudi na Waprotestanti wengi huviita apokrifa na kuvitazama kama vitabu vinavyostahili kuheshimiwa lakini si sawa na Biblia yenyewe[6].
Vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale
[hariri | hariri chanzo]Katika Biblia zinazotolewa na Kanisa Katoliki ni vitabu saba vifuatavyo (pamoja na sehemu za vitabu vya Kitabu cha Esta na Kitabu cha Danieli):
- Tobiti
- Yudith
- Kitabu cha Wamakabayo I
- Kitabu cha Wamakabayo II
- Hekima
- Yoshua bin Sira
- Kitabu cha Baruk
Baadhi ya Waorthodoksi wana vitabu vingine pia kama vile Kitabu cha kwanza cha Ezra (Ezra ya Kiebrania huhesabiwa kama Ezra 2), Kitabu cha tatu cha Wamakabayo na Zaburi ya 151; kama nyongeza Kitabu cha nne cha Wamakabayo; Ufunuo wa Ezra na hata vingine.
Vitabu hivyo vyote ama havikuandikwa (Bar, 2 Mak, Hek) ama havikupatikana mapema kwa lugha ya Kiebrania (asili kwa Sir, Judt, 1Mak) wala ya Kiaramu (asili kwa Tob), bali kwa Kigiriki tu.
Historia ya orodha ya vitabu vya deuterokanoni
[hariri | hariri chanzo]Hadi karne ya 1 KK orodha ya vitabu vya Biblia ya Kiebrania ilikuwa haijaamuliwa, ingawa ilikuwa wazi ya kwamba vitabu vya Torati ni maandiko matakatifu kamili; katika suala la vitabu vingine Wayahudi bado walitofautiana, k.mf. Masadukayo walikataa hata vile vya Manabii vilivyokubaliwa na Mafarisayo.
Sehemu kubwa ya Wayahudi nje ya Israeli na Mesopotamia walitumia toleo la Kigiriki lililoitwa Septuaginta ambalo lilitafsiriwa na wataalamu Wayahudi huko Misri katika karne ya 2 na ya 3 KK.
Kabla ya kukamilika kwa orodha ya vitabu vya Agano Jipya Septuaginta ilikuwa ndiyo Biblia ya Wakristo wa kwanza (ambao wengi wao hawakujua Kiebrania)[7][8].
Baada ya maangamizi ya Hekalu la Yerusalemu (70) na hasa katika karne ya 2 wataalamu Wayahudi, walipopatana juu ya mapokeo yao ili kujiimarisha dhidi ya Ukristo na ustaarabu wa kigeni, waliamua kutovikubali kama sehemu za Tanakh vitabu visivyopatikana kwa lugha ya Kiebrania.
Wakristo hawakufuata maazimio hayo ya Wayahudi, hivyo mwishoni mwa karne ya 2 Wakristo magharibi mwa Mediteranea walianza kutafsiri Septuaginta kwa Kilatini kilichokuwa lugha kuu kwao.
Matamko ya Kanisa Katoliki
[hariri | hariri chanzo]Vitabu vya Deuterokanoni vilihesabiwa rasmi kuwa sehemu ya Biblia hasa kuanzia Hati ya Damasi au De explanatione fidei, iliyotolewa na Papa Damasus I mwaka 382 [9].
Tafsiri ya Kilatini ya Hieronimo iliyoitwa Vulgata ilipata kuwa toleo muhimu katika Kanisa Katoliki. Hieronimo mwenyewe alipotafsiri Biblia upya katika Kilatini alisema vitabu vya Septuaginta kama Hekima, Yoshua bin Sira, Yudith na Tobiti havistahili kuwemo katika Biblia[10][11] lakini alivitafsiri ndani ya Vulgata kufuatana na maelekezo wa Papa Damaso I aliyemuagiza kazi [12]
Orodha hiyo ya Papa Damaso I ilipata nguvu Afrika Kaskazini kutokana na Agostino wa Hippo[13][14][15] kuifanya ipitishwe na Mtaguso wa Hippo (393), Mtaguso wa tatu wa Karthago (397) na Mtaguso wa nne wa Karthago (419)[16].
Wakati huohuo Papa Inosenti I aliituma kwa askofu Esuperi wa Toulouse (405)[17].
Baadaye Mtaguso wa Firenze (1442)[18] na Mtaguso wa Trento (1546)[19] ilivitambua rasmi kuwa sehemu za Biblia kamili kwa Kanisa Katoliki[20].
Misimamo ya Waprotestanti
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa Matengenezo ya kiprotestanti katika karne ya 16 Martin Luther na wengineo walishika msimamo mkali kuhusu kanuni ya Biblia akafuata azimio la Wayahudi na shauri la Hieronimo kuhusu vitabu hivyo.
Pamoja na hivyo waliweza kuweka pembeni hata baadhi ya vitabu vya Agano Jipya ambavyo zamani ulitokea wasiwasi juu yake na kwa sababu hiyo pengine vinaitwa pia deuterokanoni[21]:
- Waraka kwa Waebrania,
- Waraka wa Yakobo
- Waraka wa pili wa Petro
- Waraka wa pili wa Yohane
- Waraka wa tatu wa Yohane
- Waraka wa Yuda
- Ufunuo wa Yohane
Baada ya kifo cha Martin Luther, Waprotestanti kwa jumla walikubali tena vitabu vyote vya Agano Jipya[22] na kurudisha umoja katika jambo hilo la msingi kwa Ukristo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Bogaert, Pierre Maurice (2012). "The Latin Bible. c 600 to c. 900". Katika Richard Marsden; E. Ann Matter (whr.). New Cambridge History of the Bible; Vol II. Cambridge University Press. ku. 69–92.
- ↑ Michael D., Coogan; na wenz., whr. (2018). "The Canons of the Bible". The New Oxford Annotated Bible: New Revised Standard Version: An Ecumenical Study Bible (tol. la 5th). New York: Oxford University Press. ku. 1839, 1841. ISBN 978-0-19-027605-8. OCLC 1032375119.
- ↑ Livingstone, E. A. (2013). The Concise Oxford Dictionary of the Christian Church (kwa Kiingereza). OUP Oxford. ku. 28–29. ISBN 978-0-19-107896-5. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2020.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ International Standard Bible Encyclopedia Online. "Apocrypha". International Standard Bible Encyclopedia Online. Wm. B. Eerdmans Publishing Co. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gleason L. Jr., Archer (1974). A Survey of Old Testament Introduction. Chicago, IL: Moody Press. uk. 68. ISBN 9780802484468. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2019.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ The Popular and Critical Bible Encyclopædia and Scriptural Dictionary, Fully Defining and Explaining All Religious Terms, Including Biographical, Geographical, Historical, Archæological and Doctrinal Themes, p.521, edited by Samuel Fallows et al., The Howard-Severance company, 1901,1910. – Google Books
- ↑ J.N. D. Kelly, Early Christian Doctrines, p.53
- ↑ Stuart G. Hall, Doctrine and Practice in the Early Church, p. 28
- ↑ kwa Kilatini
- ↑ Edgecomb, Kevin P. (14 Agosti 2006). "Jerome's Prologue to Jeremiah". Biblicalia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-31. Iliwekwa mnamo 2021-07-11.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kelly, J. N. D. (1960). Early Christian Doctrines. San Francisco: Harper. uk. 55.
- ↑ "Hic prologus Scripturarum quasi galeatum principium omnibus libris, quos de hebraeo vertimus in latinum, convenire potest, ut scire valeamus, quicquid extra hos est, inter apocrifa seponendum. Igitur Sapientia, quae vulgo Salomonis inscribitur, et Iesu filii Sirach liber et Iudith et Tobias et Pastor non sunt canone. Macchabeorum primum librum hebraicum repperi, secundus graecus est, quod et ex ipsa φράσιν probari potest." (Hieronimo katika "Prologus Galeatus" au utangulizi kwa vitabu vya Samueli na Wafalme katika Vulgata)
- ↑ Everett Ferguson, "Factors leading to the Selection and Closure of the New Testament Canon," in The Canon Debate. eds. L. M. McDonald & J. A. Sanders (Hendrickson, 2002) p. 320.
- ↑ F. F. Bruce (1988), The Canon of Scripture. Intervarsity Press, p. 230.
- ↑ Augustine, De Civitate Dei 22.8
- ↑ McDonald & Sanders, editors of The Canon Debate, 2002, chapter 5: The Septuagint: The Bible of Hellenistic Judaism by Albert C. Sundberg Jr., p. 72, Appendix D-2, note 19.
- ↑ Westcott, Brooke Foss (2005). A general survey of the history of the canon of the New Testament (tol. la 6th). Eugene, OR: Wipf & Stock. uk. 570. ISBN 1597522392.
- ↑ "Eccumenical Council of Florence and Council of Basel". ewtn.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-20. Iliwekwa mnamo 2019-02-08.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ "Paul III Council of Trent-4". ewtn.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-23. Iliwekwa mnamo 2019-02-08.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ "~The Council of Trent - Session 4~". thecounciloftrent.com. Iliwekwa mnamo 2019-02-08.
- ↑ James Akin, Defending the Deuterocanonicals, EWTN, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-16, iliwekwa mnamo 2021-07-11
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Lutherbibel 1545". Bibelarbeit. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Mei 2001. Iliwekwa mnamo 5 Februari 2016.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) note order: "...Hebräer, Jakobus, Judas, Offenbarung"; see also "German Bible Versions". bible-researcher.com.
Marejeo mengine
[hariri | hariri chanzo]- Harrington, Daniel J. Invitation to the Apocrypha. Grand Rapids, Michigan: W.B. Eerdmans Publishing Co., 1999. ISBN 978-0-8028-4633-4
- Roach, Corwin C. The Apocrypha: the Hidden Books of the Bible. Cincinnati, Ohio: Forward Forward Movement Publications, 1966. N.B.: Concerns the Deuterocanonical writings (Apocrypha), according to Anglican usage.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Prophecies in the Deuterocanonical books
- Protestants defending the Deuterocanonical books
- Defending the Deuterocanonicals Ilihifadhiwa 16 Julai 2019 kwenye Wayback Machine. by Jimmy Akin
- Five common arguments Protestants give for rejecting the Deuterocanonicals (webarchive link)
- Deuterocanon Use in New Testament
- Deuterocanonical books – Full text from Saint Takla Haymanot Church Website (also available, the full text in Arabic)
- The Apocrypha: Inspired of God? Ilihifadhiwa 9 Machi 2021 kwenye Wayback Machine.
Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki
Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Deuterokanoni kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |