Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Pembetatu (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Pembetatu (Triangulum) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Pembetatu - Triangulum jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini

Pembetatu (kwa Kilatini na Kiingereza Triangulum) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu. Ni tofauti na Pembetatu ya Kusini au Pembetatu ya Kiangazi.  

Mahali pake

[hariri | hariri chanzo]

Pembetatu - Triangulum linapakana na kundinyota jirani za ) (Andromeda), Hutu (Samaki) (Pisces), Kondoo (zamani Hamali, lat. Aries) na  Farisi (Perseus):

Pembetatu (Triangulum) haikujulikana kwa mabaharia Waswahili kama kundinyota ya pekee[2]. Waarabu waliijua kwa jina la المثلث al-muthallath wakitafsiri jina lililotumiwa na Ptolemaio aliyetaja nyota hizi kwa jina la Τρίγωνον trigonon yaani pembetatu katika orodha yake ya Almagesti[3]

Awali Wagiriki waliita Δελτατων deltaton kwa sababu umbo lake linafanana na herufi ya Delta katika alfabeti ya Kigiriki. Eratosthenes alieleza hii ni ishara ya delta ya mto Naili. Katika Ulaya ilitwa kwa muda “Pembetatu Kubwa” (Triangulum Maior) kwa sababu kulikuwa pia na “Pembetatu Ndogo” (Triangulum Minor) iliyoanzishwa na Johannes Hevelius lakini hii haikuendelea. Johann Bayer aliita “Triangulum Septentrionalis” (pembetatu ya kaskazini) ili kutofautisha na Pembetatu ya Kusini[4].

Triangulum - Pembetatu ni kati ya makundinyota 48 zilizotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika kitabu cha Almagesti wakati wa karne ya 2 BK. Ipo pia katika makundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [5] kwa jina la Triangulum. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Tri'.[6]  

Nyota angavu zaidi si "Alpha" bali Beta Trianguli au Mothallah[7]. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 3.0 ikiwa umbali wa miakanuru 127 kutoka Dunia[8][9].  

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miaka nuru)
Aina ya spektra
β 4 3,00 124 A5 III
α 2 Mothallah 3,42 64 F6 IV
γ 9 4,03 118 A1 Vnn
Habari za mwangaza na umbali vinaweza kubadilika kutokana na vipimo vipya
  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Triangulum" katika lugha ya Kilatini ni "Trianguli" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Trianguli, nk.
  2. Haiko katika orodha za Knappert.
  3. PAL - Glossary Tri", tovuti ya mradi wa "Ptolemaeus Arabus et Latinus (PAL)" wa Bavarian Academy of Sciences and Humanities, iliangaliwa Oktoba 2017
  4. Linganisha Allen uk. 415
  5. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  6. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.
  7. Mothallah - Naming Stars, tovuti ya Ukia, iliangaliwa Novemba 2017
  8. Triangulum, tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
  9. Mothallah (Beta Trianguli), tovuti ya Prof. Jim Kaler

 

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

 

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 215 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331