Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Terbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Terbi (Terbium)
Jina la Elementi Terbi (Terbium)
Alama Tb
Namba atomia 65
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 158.925
Valensi 2, 8, 18, 27, 8, 2
Densiti 8.23 g/cm3
Kiwango cha kuyeyuka °K 1629
Kiwango cha kuchemka °K 3396

Terbi (terbium, pia taribi)[1] ni elementi ya kimetali yenye alama Tb na namba atomia 65, maana yake kiini cha Terbi kina protoni 65 ndani yake. Uzani atomia ni 158.925[2]. Katika jedwali la elementi inahesabiwa kati ya lanthanidi na metali za ardhi adimu.

Kiasili Terbi haipatikani kwa hali safi lakini iko ndani ya madini mengi.

Terbi ilitambuliwa kama elementi ya pekee nchini Uswidi na mwanakemia Carl Gustaf Mosander kwenye mwaka 1843. Aliikuta kama taka ndani ya oksidi ya Ytri, Y2O3. Ytri na terbi zimepokea majina yake kutokana na kijiji cha Ytterby huko Uswidi [3].

Terbium huungwa katika kampaundi za kufanya semikonda na pia kwa kuimarisha fuwele katika seli za fueli zinazotumiwa katika joto la juu.

Sehemu kubwa ya terbi inayozalishwa hutumiwa kama kimulikaji kijani, yaani dutu inaotoa mwanga kijani baada ya kupigwa kwa mnururisho fulani. Matumizi yapo katika skrini za runinga, au neli za kathodi kwa jumla.[4]

  1. Taribi ilikuwa umbo la jina lililopendekezwa na [[KAST]]
  2. Meija, Juris; et al. (2016). "Atomic weights of the elements 2013 (IUPAC Technical Report)". Pure and Applied Chemistry. 88 (3): 265–91. doi:10.1515/pac-2015-0305
  3. Elementi nne zilipokea majina yake kutokana na kijiji hicho ambako madini yake yalipatikana na kuchunguliwa: Ytri (Yttrium), Terbi (Terbium), Yterbi (Ytterbium) na Erbi (Erbium)
  4. Hammond, C. R. (2005). "The Elements". In Lide, D. R. (ed.). CRC Handbook of Chemistry and Physics (86th ed.). Boca Raton (FL): CRC Press. ISBN 978-0-8493-0486-6.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Terbi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.