Yamoussoukro (mji)
Jiji la Yamoussoukro | |
Nchi | Cote d'Ivoire |
---|---|
Jimbo | Yamoussoukro |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 355,573 |
Tovuti: yamassoukro.org/en/ |
Yamoussoukro ni mji mkuu rasmi wa Cote d'Ivoire tangu 1983 ilipochukua nafasi hii kutoka Abidjan inayoendelea kuwa mji mkubwa na kitovu cha kiuchumi pia kiutamaduni na makao ya ofisi nyingi za serikali. Iko takriban 230 km kutoka pwani karibu na kitovu cha nchi. Kuna wakazi 355,573 (mwaka 2014).
Historia ya mji
[hariri | hariri chanzo]Chanzo cha Yamoussoukro ni kijiji kidogo kilichoitwa N'Gokro. Imeteuliwa kuwa mji mkuu na kukua kwa sababu ni mahali pa kuzaliwa kwa rais wa kwanza wa nchi Félix Houphouët-Boigny. Mwanzo wa ukoloni wa Kifaransa kijiji cha N'Gokro ilikuwa chini ya chifu wa kike Yamousso. Mwaka 1909 kabila la eneo hili liliasi dhidi ya Wafaransa lakini sehemu ya machifu pamoja na Yamousso waliwashauri wenzao kupatana na Wafaransa tena. Tendo hili lilisababishwa Wafaransa kuhamisha kituo chao cha kiutawala wa eneo kwenda N'Gokro wakiita Yamoussoukro kwa heshima ya chifu yake.
Aliyekuwa rais baadaye Félix Houphouët-Boigny alizaliwa Yamoussoukro mwaka 1905. 1939 akawa chifu wa mahali akaendelea kujishughulisha na siasa na kuita mikutano wa machifu akiwaalika kwake kijijini. Baada ya kuwa rais wa Cote d'Ivoire mwaka 1960 aliamuru tangu mwaka 1964 kazi nyingi zifanywe kwake nyumbani kama ujenzi wa ikulu yake ya pili, majengo mengine ya umma, barabara, kituo cha umeme, viwanda, uwanja wa michezo na mengi mengine. Kelele ya ujenzi ilikuwa Kanisa Kuu la Yamoussoukro lililojengwa kwa mfano wa Kanisa la Mt. Petro huko Roma lakini kubwa kuliko kanisa lile linalotumikwa na Papa mwenyewe.
Mwaka 1983 ilitangazwa rasmi kuwa mji mkuu lakini ofisi nyingi za serikali na wizara bado zimebaki Abidjan.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Yamoussoukro (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |