Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Hakuna Jinamizi Nje: Ni Kirusi Placidius Ndibalema Fredrick M. Nafukho Machuma A. Muyia Beverly J. Irby Rafael Lara-Alecia Nahad Abdelrahman Fuhui Tong Pam Schiller Illustriert von Debbie Weekly ISBN 978-1-7358505-0-4 90000> 9 781735 850504 Hakuna Jinamizi Nje: Ni Kirusi Placidius Ndibalema Fredrick M. Nafukho Machuma A. Muyia Beverly J. Irby Rafael Lara-Alecia Nahad Abdelrahman Fuhui Tong Pam Schiller Illustriert von Debbie Weekly Tafsiri ya Kiswahili na Placidius Ndibalema © 2020 Herausgegeben von Center for Research and Development in Dual Language and Literacy Acquisition, Department of Educational Psychology, College of Education and Human Development, Texas A&M University Nazisikiliza taarifa na kuzitafakari. Kuna jinamizi nje, na sasa siwezi kucheza. Ninachungulia dirishani, lakini silioni jinamizi. Kwa dakika hivi, najawa na furaha. Lakini bado sioni marafiki nje wakicheza. Hakuna marafiki wanaokimbiakimbia, wanaoendesha baiskeli, wanaorukaruka au wanaokimbizana. Kwenye taarifa ya habari tunasikia, “Vaa barakoa.” “Ni jinamizi gani linaogopa barakoa?” Nauliza. Baba anasema “Inawakinga wengine” “Oh,” Nasema. “Kama marafiki zangu, dada zangu, na kaka zangu?” Kuanzia nyuma ya mlango, naangalia kote. Sioni jinamizi angani, na hata aridhini. Taratibu, nakagua chumbani kwangu-Je, limejificha humo? Hapana-sioni vidole wala sura ya jinamizi hilo. Pole pole, nachungulia chini ya shuka langu jeupe Sioni kope za jinamizi wala unyayo wake. Halipo chini ya kiti changu. Wala sakafuni. Halipo chumbani kwangu. Wala nyuma ya mlango. Mama anasema, “Osha mikono yako kama ilivyo kwenye wimbo wa siku ya kuzaliwa.” “Kimsingi, imba wimbo huo mara mbili.” Nashangaa, “Kwa nini muda mrefu?” Mama anasema, “Usiguse uso wako safisha uso wako ili kuondoa vijidudu vyote Ni muda wa kwenda kulala, naangaliaangalia pembeni tena. Kwa bahati nzuri- sijaliona jinamizi. Katika ndoto zangu-hakuna jinamizi linalotokea Lakini hii hainiondoleihofu Namwambia mama yangu kuhusu ndoto yangu; najua ataelewa. Anacheka na kisha kunishika mkono. Anasema “Ni kirusi, na wala sio jinamizi, ….. Mara tu kirusi hiki kikiondoka, wewe na marafiki zako mnaweza kwenda nje kucheza.” Mama ananiambia, “chukua tahadhari na usiogope. Pamoja na barakoa na glovu zetu, kwa sasa tujifanye kama tupo kwenye gwaride” “Madaktari na wanasayansi wanafanya kazi usiku na mchana Kutengeneza chanjo ambayo itakiondoa kirusi hiki” Pia nasema kwa uafadhali mkubwa “hakuna jinamizi nje-hakuna jinamizi la kuogopa. Niko imara kabisa, kwa kuwa hakuna jinamizi karibu yangu.” Ujumbe Kuhusu Kitabu Hiki Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya watoto ambao wamesikia habari juu ya virusi vya COVID-19 ambavyo vimesababisha waishi Virusi vinaweza kukufanya uugue usipochukua tahadhari wala kujikinga. kwa hofu. Maranyingi tumekuwa tukisikia hadithi za watoto wakisimulia juu ya kuchukulikwa na watu wabaya na Jitafakari kwa kila utendalo, na utakuwa salama. Fuata njia rahisi za kujikinga. kupelekwa mbali na familia zao, vitu vya ajabu ambavyo vimetokea madarasani kwao, marafiki zao waliopotea au kushikwa na jinamizi. Hofu yote hii imekuwa ikielezwa katika ndoto za usiku na mchana za watoto tunaowafahamu. Hiki kitabu kinaleta matumaini yetu ya baadae-watoto wote duniani-na familia zao na walezi wao. Ni matamanio yetu kitabu hiki kiwaletee watoto faraja na amani Safisha mikono yako mara kwa mara kila siku. Epuka kugusa uso wako. Vaa barakoa ukiwa karibu na wengine. Kaa umbali wa angalau mita sita kati yako na mtu mwingine. katika kipindi kigumu. Kitabu hiki kimechapishwa katika kwa lugha mbalimbali kukidhi hitaji la kujisomea katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya korona. Kitabu hiki hakiuzwi, kimedhaminiwa na kituo cha Utafiti na Maendeleo katika lugha na ukuzaji wa kusoma na kuandika, Idara ya Saikolojia, Ndaki ya Elimu na Makuzi ya Binadamu, Chuo Kikuu cha Texas A&M. Na yawepo mazuri tu ndani na nje ya ulimwengu wa watoto wetu! Mimi na wewe, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko! Placidius Ndibalema Fredrick M. Nafukho Machuma H. A. Muyia Beverly J. Irby Rafael Lara-Alecio Nahed Abdelrahman Fuhui Tong Pam Schiller