Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Parafujo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Parafujo mbalimbali
Skurubu ya ubao
Bolti na nati

Parafujo (kutoka Kireno parafuso; pia: skurubu/skrubu kutoka Kiing. screw; pia bolti kutoka Kiing. bolt kama inatumiwa pamoja na nati) ni kifaa kinachofanana na msumari kinachotumika kuunganisha vipande viwili. Tofauti na msumari nondo yake ina hesi kando lake; upande wa juu kuna kofia inayotumiwa kuikaza au kuifungua.

Kama vipande viwili vimeunganishwa kwa kutumia skurubu ni rahisi kuzifungua tena.

Kwa kawaida parafujo hutengenezwa kwa metali lakini kuna pia skurubu zilizotengenezwa kwa plastiki na ubao.

Kwa jumla parafujo au skurubu zinatofautiana kutokana na madhumuni yao yaani aina ya maunzi yanayoshikwa nazo. Kuna aina tatu

  • parafujo inayokata njia yake katika maunzi laini kama ubao au plastiki
  • parafujo inayoingia katika nafasi iliyoandaliwa yenye hesi ya kike ndani yake inayolingana na hesi ya skurubu
  • parafujo inayopita katika shimo ikishikwa nyuma kwa nati yenye hesi ya kike ndani yake. Aina hii huitwa pia bolti.

Skurubu ya ubao ina kazi ya kuunganisha vipande viwili vya ubao. Huwa na umbo la pia maana yake inaanza nyembamba na kuwa pana zaidi hadi chini ya kofia yake. Sehemu ya mwisho chini ya kofia mara nyingi haina hesi.

Hesi inakata njia yake katika ubao; kama ubao ni ngumu au nene mara nyingi shimo ndogo inatangulia kutobolewa kwa keekee. Shimo hili lapaswa kuwa nyembamba kuliko skrubu itakayopita baadaye. Skurubu za aina hii huwa na kofia yenye tundu ama nyoofu au yenye umbo la msalaba. Bisibisi inayolingana na tundu hutumiwa kugeuza parafujo.

Parafujo kubwa za kushikilia sehemu mbili inahitaji nati. Hesi yake haitakiwi kukata njia yake; pande mbili zinazotakiwa kushikwa na skrubu hii zimetobolewa shimo ambamo parafujo inapita bila tatizo; kofia inakaa upande mmoja na mwisho wa skrubu mwenye hesi unatoka upande mwingine. Hapa nati inafungwa na kukazwa.

Aina hii hutumiwa kushika ama vipande viwili vikubwa vya ubao au pia sehemu za mashine yenye mwendo na mtetemo. Kofia yake kwa kawaida huwa na kona sita ikigeuzwa kwa kutumia spana.


Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Parafujo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.